Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

2.5.19

WhatsApp Inaendelea Kuwazuia Watumiaji ambao wanatumia 'GBWhatsApp'.


Image result for gb whatsapp


Whatsapp ni programu rahisi sana kupata. Ipo katika Vifaa yote vyenye mifumo endeshaji ya simu janja.

Hata hivyo bado utapata Nakala za  Whatsapp kila mahali na mojawapo ya Nakala maarufu inaitwa GBWhatsApp. Kiukweli inaonekana Whatsapp Haijafurahishwa sana juu ya hili tofauti na watu wanavyo ifurahia hii programu.

WhatsApp Inaendelea Kuwazuia Watumiaji  ambao wanatumia 'GBWhatsApp'.
    Na Baadhi watu hao ni @Anandaji kutoka twitter ambao ame share Nasi Kwa picha jinsi gani kakutana na changamoto hii.
Maandishi yanasomeka: Umekatazwa kwa muda kutumia Whatsapp kwa sababu huenda umevunja masharti yetu ya huduma. Ujumbe huo ulifuatiwa na sticker ambayo ilionyesha muda gani WhatsApp imekuzuia , ambapo katika kesi hii, mtu huyu alipigwa marufuku kwa saa zaidi ya 9!


Ukiangalia Masharti ya Huduma ya WhatsApp, unaweza kuona sehemu nyingi ambapo GB Whatsapp imevunja masharti yao.

Chini ya 'Haki za Whatsapp', inasema: Tuna haki za hakimiliki, alama za biashara, domains, nembo, mavazi ya biashara, siri za biashara, ruhusa na haki nyingine za haki za urithi zinazohusishwa na Huduma zetu. Huwezi kutumia haki miliki zetu, alama za biashara, domains, nembo, mavazi ya biashara, ruhusa, na haki nyingine za urithi isipokuwa uwe una ruhusa yetu ya kibinafsi na ila kwa mujibu wa Mwongozo wa Brand.
 
Soma vigezo na masharti Ya Whatsapp Hapa

Hii inaweza kuwa sababu ya Kwanini WhatsApp inawapiga marufuku kwa muda watumiaji kutumia GBWhatsApp. Hatua ya kupiga marufuku watumiaji wanao tumia Whatsapp GB inaweza pia kuwa hoja ya fujo ya Whatsapp ili kuwakata tamaa watu kutumia GBWhatsApp na kutumia programu rasmi.

Kuna vifungo vingi vya Whatsapp huko nje na tunapaswa kuona kama hii ni mwanzo wa mwenendo wa Whatsapp ili kudhuia kila moja kutumia nakala badala ya programu rasmi.

                                      Image result for gb whatsapp


GBWhatsApp Ina vitu vingi vizuri kuliko Hata Whatsapp Maalumu.
Uwezo wake ni Mkubwa kwani unavingi vya kutumia ambavyo whatsapp maalumu imeshindwa kuwekewa ndani ya programu hio.

Ukiwa una GBWhatsapp Utaweza kufanya ya fuatayo.

Utaweza kuficha Last seen Yako.
Utaweza kuficha tiki za Bluu (zinazoonyesha kama ujumbe umesomwa)
Utaweza kujificha unapotazama Status ya mtu.

 Na mengine mengi utayakuta huko.