Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

23.4.19

Toleo jipya lijalo kutoka WhatsApp linaweza kuzuia watumiaji kuchukua screenshot ya mazungumzo yao binafsi.

                          Image result for whatsapp lock

WhatsApp inaripotiwa inafanya kazi kwenye sasisho ambalo linaweza kuzuia watumiaji kupiga picha za skrini za mazungumzo yao.

Programu ya ujumbe maarufu ulimwenguni, inayotumiwa na watu zaidi ya bilioni kila siku, inasasishwa mara kwa mara, ina maana kwamba vipengele vipya vinazidi kuwekwa daima.


Kwa mujibu wa WABetaInfo, WhatsApp sasa inatazama kipengele cha usalama cha vidole vidogo (fingerprint).

                    Image result for whatsapp fingerprint

Kipengele hicho kitaruhusu watumiaji kuwezesha uthibitishaji wa vidole  ndani ya Whatsapp, maana watumiaji watahitajika kuweka  alama za vidole vyao ili kufikia mazungumzo yao.


Programu itahifadhiwa kabisa, hivyo mtumiaji atahitaji kuthibitisha utambulisho wake wa vidole ili kufungua Whatsapp, "WABetaInfo ilielezea  Januari Mwaka huu.

"Alama za vidole hizo zitakuwa za kulinda programu nzima, Nasio kufungia mazungumzo baadhi."


Chanzo:WABetaInfo