Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

9.4.19

Sarafu:App ya kufanya manunuzi mtandaoni ya Azam

Azam imekuwa kampuni kubwa saba Tanzania katika nyanja mbalimbali, miaka ya nyuma ilijulikana kwa utengenezaji wa bidhaa za kula tu, lakini kwa sasa ni habari nyingine.

Kutokana na kujiongeza kwa kwao, kwa sasa wameamua pia kujiingiza kwenye teknolojia. Ndio maana unaona kuna azam tv, ving'amuzi vya azam na azam tv App.


Kampuni hii imebuni app ingine inayoitwa SARAFU, hii imeletwa mahususi kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za azam kwa wafanyabiashara wa aina zote. Kama ni mfanyabiashara mdogo unaweza kuagiza mzigo na ukaletewa mpaka ulipo bila malipo.


Faida ya app hii ni kupata bei zile toka kiwandani kabisa na kusafishiwa bure.
 
    JINSI YA KUJIUNGA

  • Uwe na simu janja
  • Pakua SARAFU app
  • Jiandikishe kwa usahihi
  • Agiza bidhaa kwanzia 70,000

Ukiagiza bidhaa utachagua eneo ulilopo ili waweze kuona(currently location) malipo ni kwa njia ya mobile money yani kama tigo pesa, benki n.k. Baada ya saa 2 mpaka 3 utaletewa mzigo wako.

Endelea kutufuatilia kwenye mitandao ya kijamii telegram, Facebook Twitter na Instagram pia.