Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

24.4.19

Kwa nini Nambari Yako ya Whatsapp Inazuiliwa kutumia Whatsapp ? Na Jinsi ya kurejesha Namba yako itumie tena Whatsapp.

                              Related image
Akaunti yangu ya WhatsApp imefungwa kwa kupigwa marufuku kisha kuonyesha "Namba yako ya simu imepigwa marufuku  kutumia Whatsapp. Contact support for help ". Nifanye nini sasa?
   Katika makala hii, unaweza kujua juu ya makosa uliyofanya ambayo yame kusababishia WhatsApp akaunti yako kupigwa marufuku. Hebu tujadili kila kitu kwa undani zaidi.
 
                       
                             Related image


 Whatsapp ni programu ya ujumbe wa papo inayotumiwa na mamilioni ya watu hii leo, kuna nafasi nyingi ambazo mtu yeyote anaweza kuitumia vibaya programu hii. Ikiwa utaitumia akaunti yako kwa shughuli na matumizi mabaya tofauti na mfumo waona utakuwa umeweza kukiuka masharti na hali, hivyo akaunti yako itapigwa marufuku kwa muda kuto tumia Whatsapp.

Kuna sababu maalum mpaka unapigwa marafuku unapokiuka katika kufuata sheria za WhatsApp . Ukosefu wa kufuata maelekezo ya kusoma kabla ya kuanza kutumia Whatsapp, Hilo ni kosa la kwanza ulilofanya. Hapa nimeandika sababu za kwanini Whatsapp ina kuzuia.

    Hapa kuna baadhi ya sababu ambazo zinaweza kusababisha wewe kupigwa marufuku kutumia Whatsapp.


-> Kutuma ujumbe kwa wingi kwa anwani zisizochaguliwa (Sending bulk messages to unlisted contacts)
-> Kushare Link za tovuti na link zenye matangazo kwa wingi kwa siku(Sharing website URLs and ad links for multiple times a day)
-> Kutengeneza vikundi vya Maudhui ya ngono na picha za kiutu uzima (Creating porn & adult-related groups and broadcasts)
-> Kuzuia Nambari yako ya Whatsapp kwa watu wengi.(Blocking your WhatsApp number by many people)
>Kutumia Mods za whatsapp tofauti na Whatsapp Maalumu(Hii ni sheria Mpya ambayo bado inafanyiwa kazi japo imeshaanza kufanya kazi mpaka sasa kwa baadhi ya watu ambao wamekaa mda mrefu wakitumia hizo mods bila kutumia whatsapp maalumu).

>Idadi nyingi ya watu wana ripoti Namba Yako kwa Matumizi mabaya (Unaboa watu)

                         

   > Wakati mwingine whatsapp wanakuzuia kwa sababu fulani, Whatsapp inaweza kukupiga marufuku wewe kutumia akaunti yako kwa kipindi cha muda kama vile saa 72. Kuna Baadhi ya watu wengine nilisikia wakisema "WhatsApp ilizuia nambari yangu kwa saa 72", baada ya hapo akaunti ililejea moja kwa moja.      Jinsi ya kuepuka marufuku ya Whatsapp &    Jinsi ya kurejesha Namba yako itumie tena Whatsapp.
           

Je, ulifanya makosa zaidi ? Usiwe na wasiwasi, nina njia bora za kutatua Tatizo hilo.
 Fuata hatua zilizo chini hapa :

-> Futa (unistall) Whatsapp yako iliyopo sasa.
-> Pakua na install Whatsapp yenye  toleo jipya.

-> Ingiza namba yako ya simu na utaona Maelezo kama screenshot hii inavyoeleza.

>Bofya kwenye sehemu ya  “Support” 
->Fomu ya mawasiliano ya msaada itakuwa kama hapo
->Andika tatizo lako na piga screenshot ni aje whatsapp  inakwambia
->Usisahau kuweka Nambari yako hio
->Bofya “Next” Na shuka chini
->Chagua “This does not answer my problem
->Sasa tuma kwenye Email ya usaidizi wa whatsapp  support@whatsapp.com
->Baada ya masaa 4 angalial inbox ya Email yako. Utaona WhatsApp reply na maelekezo ya nini ufanye .


NB: KAMA HUTOPATA REPLY YOYOTE KUTOKA WHATSAPP JUA NAMBA YAKO IMEKULA BAN LA JUMLA HIVO TAFTA NAMBA NYINGINE KISHA SAJILI.