Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

31.3.18

[DEEP WEB NA DARK WEB]ULIMWENGU MWENGINE WA MTANDAO WA INTANETI

   Leo tumewawekea makala ambayo inaweza kuwa ngeni masikioni mwako, huwenda ushawahi kusikia lakini hukuekewa vizuri, leo soma kwa undani ili ujifunze.

Pamoja na Injini pekuzi(Seach Engine)kukupa matokeo mengi ya vitu unavyotafuta mtandaoni unajua kuwa sio vyote?

 Je wajua kuwa ipo sehemu ya mtandao wa intaneti iliyofichwa? Ambayo ni Deep web na Dark web? Twende pamoja.

              DEEP WEB NI NINI?
Deep web ni sehemu ya intaneti ambayo haionekani kwenye injini pekuzi kama vile Google,Yahoo na Bing  moja kwa moja injini pekuzi haziwezi kuona sehemu hii kwa sababu imefichwa isionekane.
 Deep web siyo kitu cha usichokijua kabisa bali ni kitu ambacho umekuwa ukikitumia mara kwa mara kama barua pepe yako, benki mtandao, meseji zako za Twitter,facebook n.k,Taarifa hizi haziwezi kuonekana kwenye injini pekuzi kwa kuwa zinalindwa kwa nywila (password) au kulipiwa ili kuziona.

 Vitu vyote visivyopatikana kwenye uso wa juu wa mtandao kwa kutumia injini pekuzi ni sehemu ya Deep web, Ikizingatiwa kuwa tuna mabilioni ya watumiaji wa mtando wa intaneti duniani, hivyo inaelezwa kuwa kuna mamilioni ya taarifa au data zilizoko kwenye Deep web.

Hata hivyo inaminika kuwa Deep web inaunda sehemu kubwa ya mtandao; Deep web inaweza kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida kama vile Chrome na Firefox.

      DARK WEB NI NINI? 
Mtandao maarufu kwa biashara haramu 

 Dark web siyo sehemu tofauti na intaneti bali ni sehemu ya Deep web ambayo haiwezi kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida.

Kwa nini Dark web haiwezi kuonwa kwa kivinjari cha kawaida? Ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web ni haramu, si rahisi wahusika wake kuruhusu mambo haya kuonekana kwenye vivinjari vya kawaida, ndio maana kuna usiri mkubwa kuliko deep web. Pia kuna ijini pekuzi ya kipekee kwa ajili ya kutafuta hukobkama  ilivyo kwa Google ambayo ni https://duckduckgo.com .

Je kwenye Dark web kuna shughuli gani?
Biashara zinazofanyika kwenye dark web

  • Uuzaji wa madawa ya kulevya
  • Uhalifu wa kila namna (uuzaji wa viungo vya binadamu, ajira za kutisha, ugaidi n.k)
  • Wadukuzi hatari wa kompyuta
  • Uuzaji wa taarifa na vitu vilivyoibiwa
  • Picha za unyanyasaji wa kingono hasa watoto
  • Uuzaji wa silaha
  • Mawasiliano ya wanaharakati na waandishi wa habari wanaotaka kuibua maswala mbalimbali. Hutumia njia hii kujificha wasije wakakamatwa na serikali au mahasimu wao. Mtandao wa wikileaks unapokea pia taarifa kupitia Dark web.
Je tovuti za Dark web zinaperuziwaje?
 Tovuti za Dark web zinaishia na anwani mtandao (domain) zenye .onion, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia kivinjari cha Tor pekee.

Tor ni kivinjari cha namna gani?
  •   Tor ni kivinjari kilichotengenezwa na watu wakujitolea (voluntiers) kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambacho hufanya kazi kwa usiri wa hali ya juu wa kuficha mawasiliano pamoja na watumiaji wake. Ukiwa kwenye kivinjari hiki hautaweza kupiga picha ya kioo(screenshot kamwe) 
  • Wala kupakua video au picha, utaangalia na kuacha hapo tu

Hivyo mtu anayetembelea tovuti fulani au kufanya chochote kwenye mtandao kwa kutumia kivinjari hiki siyo rahisi kubainika.
Kwa mfano unaweza ukawa unaperuzi mtandao kwa kutumia Tor ukiwa Tanzania lakini ukaonekana mara uko Japan, mara Uingereza au hata Marekani.[kama VPN]

Ikumbukwe kuwa kutembelea Dark web siyo kinyume cha sheria lakini kufanya vitu huko kunaweza kuwa kinyume cha sheria kutokana na tovuti nyingi kufanya vitu vinavyokiuka sheria.
Kwenye Dark web siyo mahali salama  kama sehemu ya kawaida ya mtandao wa intaneti tulio uzoea. Tovuti nyingi huku zimetengenezwa kwa makusudi maalumu au pengine ya siri, hivyo hazikujali wala kukulinda.

Ili kuperuzi kwenye Dark web ni lazima uwe na kiungo (link) cha tovuti unayotaka kutembelea kinachoishia na .onion kwa mfano
[silkroad7rn2puhj.onion]

Je Dark web ni mbaya?
Hapa kuna majibu mawili ndiyo na hapana. Pamoja na kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web sio halali, bado kuna toleo lake la Facebook na ProPublica kwa anauani ya .onion.
Lakini ukumbuke kuwa wachambuzi wa mambo wanasema tovuti hizi zinaweza zisiwe za kweli, kwani si rahisi Fecebook kukubali watumiaji wake kutumia anwani za kujificha za .onion. Hivyo kuwa makini na taarifa zako za siri huku.

  Uzuri wa Dark web ni kuwa inawawezesha waandishi wa habari, wanaharakati na wale wanaoibua taarifa za siri kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila wao kujulikana.
Ni wazi kuwa hakuna kitu kibaya kwenye mtandao bali ni matumizi pekee ndiyo hukifanya kiwe kibaya.

     USHAURI KWA WATUMIAJI
Dar web si mbaya ila ubaya wake matumizi yake, kama huna kazi au matumizi na hii sehemu, usitumie, na kama utatumia Hakikisha umeziba kamera zako iwe kwenye laptop au simu. Epuka kujaza taarifa zako nyeti kama za bank na sehemu zingine.        Chanzo ni JamiiForums