Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

21.3.18

APPS ZA GOOGLE ZILIZOSHINDWA SOKONI


Google ni kampuni iliyojitosheleza kila idara,pamoja na uwezo wao wa kuunda apps tumizi zenye faida kama Ramani,Tafsiri,Chrome,Youtube n.k,lakini pia wana apps zilizoshindwa sokoni.

Hizi apps tumezileta hapa kutokana na hata viwango (rate)vyake kwenye soko la Google Play.
 Apps nzuri lazma iwe na makadirio mazuri sokoni, kama kwanzia nyota 4 kwenda juu.

   Google  Hangouts.:-Hii imetkka mbali sana,mwanzoni ilikua unajuliakana kama Google talk, ikakosa upendezi, ikafanywa kuwa Messengeplus bado haikufua dafu na mapinduzi makubwa yakafanywa kutokana na Ilivyokuja WhatsApp, app hii ikapewa uwezo wa kuchat online kama WhatsApp na pia kutuma ujumbe mfupi,lakini bado haijawashawi watu wengi kuipenda. [4.0 viwango playstore]

 Google Play Music:-Hii ni kichezaji[player]kwa muziki, app ni ya muda lakini kutokana na soko la apps kuwa na ushindani mkali app hii imekosa mvuto kwa watumiaji wa wake, simu ya Android zinapokuja zinakuja na app ya kucheza mziki,na pia hii na Google huenda hii ndo inayochangia kukosa upendezi, kingine katika hii app, haina kucheza nyimbo kwa folda, hii inachanganya nyimbo zote kwa pamoja, wakati watu wanapenda kucheza aina fulani kwa kupanga, kama ni hip hop pekee na afropop kivyake, lakini ukiwa na app hii huwezi kutemganisha hivyo.[ 3.9 viwango playstore]

Google Play Movies&Tv:-Hii app huenda ni kwa TZ ama Afrika lakini sijawahi hata kufanikiwa kuona faida yake,na movies nyingi kule zinauzwa tena bei kubwa, kukodi tu movie 1 inakadiriwa kuwa ni Tsh4000,[3.7 viwango  playstore]

Google Play Newstand:-Hii ni kwa ajili ya kukupa habari za magazeti na majarida mbalimbali maarufu,kaa hapa Afrika hatujapata pendeleo la kuwekwa gazeti au jarida kubwa kama ilivyo kwa wenzetu,huwenda kutokana na eneo ndio mana imechangia app hii kukosa mvito kwa watumiaji, hasa kwa Afrika na Asia. [3.9 viwango playstore]

Kuna zilizosahaulika hapo? Karibu telegram tubadilishane mawazo Smatskills