Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

11.2.18

NJIA TANO ZA KUPAKUA VIDEO YOUTUBE KWA URAHISI

 Hakuna asiependa kuhifadhi video kwenye simu yake ili aweze kuangalia badae akiwa nje ya mtandao,lakini nawezaje kuhifadhi video za YouTube kwenye kifaa changu?

SOMA PIA:SIRI MUHIMU ZA TELEGRAM

 NJIA 5 RAHISI ZA KUPAKUA VIDEO YOUTUBE


 1.TUBEMATE:- Hii ndio njia maarufu na kongwe katika mambo ya kupakua video YouTube,njii ilianza kufanya kazi toka 2011 katika toleo la Android 2.2,wakati huo soko maarufu ukiachana na Android market ilikuwa ni GetJar.
 Ukiwasha tu app ya tubemate na moja kwa moja itakuelekeza kwenye YouTube.

2.SNAPTUBE:- Hii sio YouTube bali hata kwenye mitandao mingine kama Facebook,instagram na baadhi ya mitandao mingine ambayo sio maarufu sana. Hii ilipendwa kutokana na mjumuiko wa mitandao yote.

3.VIDEODAR:- Hii haina umaarufu mkubwa sana,lakini inakuja kwa kasi kutokana na wepesi wake wa kupakua video,hii ni site nyingi kuliko zingine. YouTube, Facebook, Twitter insatgram,vimeo soundclouds na mingine mingi tu

4.UC BROWSER:- licha ya kupakua video tu, ni kivinjari kizuri sana kwa matumizi ya aina zote, hii licha ya kupakua video YouTube hata nyimbo za kusikiliza mtandaoni(online)ukiwa na uc inakupa chaguzi ya kupakua au kusikiliza huko huko.

5.SAVEFROM.NET:- Hii nzuri kwa wasiopenda kijaza simu zao mambo mengi, yan hii sio app, ni njia rahisi sana ya kupakua video YouTube kwa kunguza ile url na kuongeza ss.
  Iko hivi tumia Kivinjari chochote kwenye simu yako kwenda YouTube, tafuta video unayotaka ukishaiona hariri ile link juu(mfano ipo hivi https://m.youtube.com/watch?v=HXh1PzYEYNM)
wewe ipunguze iwe hivi [ssyoutube.com/watch?v=HXh1PzYEYNM] piga Go hapo utaona video yako inaanza kujipakua

Angalia hii video fupi jinsi ya kupakua


Kama kuna swali karibu kuuliza kwenye maoni chini, kama uko telegram karibu kwenye channel yetu👉 Smatskills Official