Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

16.2.18

KUWA MAKINI NA MAMBO HAYA USIIBIWE SIMU YAKO

 Smatskills tulishaandika jinsi ya kutafuta simu iliyoibiwa, endapo tu kama utakuwa uliiwekea apps za kuifuatilia.


  ULIWAHI KUPOTEZA SIMU?JE KWA NJIA GANI?
  1. Uliibiwa? 
  2. Uliporwa?
  3. Ulichomolewa?
  4. Ulitapeliwa?
  5. Uliangusha? 
SOMA PIA:JINSI YA KUTAFUTA SIMU ILIYOIBIWA

Bila shaka lazma kuna nia moja wapo hapo juu uliwahi kutumika kwa kupotea simu yako. Leo tunakupa mapendekezo ya jinsi ya kushika simu yako pale unapokuwa matembezi kwenye mji wenye shughuli nyingi. 

KWANZA KUWA MAKINI NA HAYA

  • Unapotembea njiani, ni vyema ukashika simu yako mkononi na usiruhusu mtu akubane bane kila wakati.
  • Ikitokea umekanyagwa na mpita njia mwengine usizozane nae hata kidogo, kuwa mjinga na usonge mbele(mzozo utakupumbaza na itakuwa rahisi kuchomoloewa simu yako).
  • Ikitokea wewe ndio umemkanyaga mpita njia, wala usisimame kuongea sana, omba msamaha kwa kunyoosha mkono na uendelee na safari(wezi wengi hujitega njiani ili wapate sababu ya kukanyagwa). 
  • Mtu yeyote atakae kushika au kukutingisha akidai "TEMBEA VIZURI WEWE"kama uko vizuri mtandike na usonge, kama hutaki mzozo kazia fikra mifukoni mwako(hapo anakutoa ufahami ili uwazie tukio na ujisahau kwenye mifuko yako).


KAMA UMESOMA KWA MAKINI ITAZINGATIA, NA KUMBUKA MWIZI HATEMBEI PEKE YAKE, WAKO ZAIDI YA MMOJA.

matukio yaliyo elezwa juu hapo hufanywa na mmoja wakati huo mwengine ndo anashughulika na mifuko yako, unaweza kufika mbele ukajikuta huna baadhi ya vitu mifukoni mwako hasa simu.