Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

6.2.18

Keyboard tano bora za kutumia kwenye simu yako

Hakuna kero kubwa kama dictionaries kwenye vicharazio(keyboard) vya simu,hii hutokea pale unapotaka kuandika kitu fulani basi yenyewe inabadilisha na kuweka vingine.
Japo huwa inatokana na lugha ya kiingereza mara nyingi unaweza kubadilisha na ku tune off(kuzima). Leo nataka nikupe vicharazio vitano ambavyo ni bora kabisa kutumia bila usumbufu.

           Gboard

Hiki ni kinatengenezwa na Google sifa zake

 1.        Themes nzuri
 2.        Dictionaries nyingi ikiwemo ya Kiswahili
 3.        Number row(namba zikae juu)
 4.       Google search hapo hapo
 5.       Emoji nyingi n.k
Binafsi natumia hii,ukiitaka pakua hapa Gboard

      Touch Pal

Hii ni maarufu sana kwa sasa,na hii inatokana na kuja na simu nyingi za Tecno ikiwa kama officials keyboard.

 1.       Theme tofauti tofauti
 2.       Dictionaries nyingi kiswahili pia kipo
 3.       Number row
 4.       One hand mode
 5.      Shake to move (Unaweza kuweka sehemu utakayo,iwe kati juu kidogo pembeni vyovyote)
 6.       Emojis,Gif 
 7.       Font styles
Matangazo ndio yatakuwa kero kwako.ipakue hapa kama umeipenda Touch Pal

      Kika keyboard


Hii haina mambo mengi sana sema iko fasta na ina muonekano mzuri pia kama zingine haina matangazo.

 1.      Emojis
 2.      Font styles
 3.      Dictionary pia haina kiswahili

Kama umeipenda ipakue hapa Kika keyboard

  iKeyboard 

Hii ni keyboard mataya sana haiko playstore lakini ina muonekano wa vicharazio vya iphones,kama unaitaka unaweza kuipakuwa hapa iKeyboard


     Xperia Keyboard.               Samsung Keyboard
Hii inakuja na simu za Sony.       Simu za Samsung