Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

7.2.18

Kero na Changamoto kwenye makundi ya WhatsApp

Miongoni wa app yenye watumiaji wengi na iliyopakuliwa mara nyingi kwenye soko la Google play ni WhatsApp,mpaka sasa imepakuliwa zaidi ya mara bilioni 1½.

  Kwa asilimia nyingi watu wana makundi tofauti kwenye simu zao,unaweza kuwa na kundi la ufugaji, dini, teknolojia na hata vichekesho,umewahi kukutana na kero au changamoto hadi kuona kundi halina maana tena kwako? Twende pamoja.

  FAIDA ZA MAKUNDI HAYA

1)Kwanza kabisa ni kuwaweka watu karibu:yaani mnaweza kuwa mbali mbali kieneo lakini kupitia vikundi hivyo mkaweza kuwa pamoja na kujadili mambo yenye tija kwenu.

2)Kujifunza mambo ‎mbalimbali kupitia simu yako: unaweza kuwa ulikua hujui kupika, ila kupitia kundi la mapishi ukajifunzia huko na ukajua,hiyo ni faida,vivyo hivyo kwa IT, Vichekesho burudani na mengineyo.

Soma pia:Jinsi ya kufuta ujumbe uliozidi dk 7 WhatsApp 

KERO NA CHANGAMOTO ZAKE

1)Ubabe kwa viongozi: pamoja na kundi kuwa na sheria lakini wanachama huona kama hazina uzito,atakayevunja na kutolewa hujiona kama kaonewa hivvyo migawanyiko huanza kundini na hata uasi.

2)Umeungwa kwenye kundi usilopenda: watu wenye no zako ni wengi au wengine huenda wamekuona kwa kundi lingine na kuamua kukuweka kwenye kudni lao,inaleta usunbufu sana.

3)Kushindwa kujitoa kwa sababu ya kumogopa kiongozi:hii inatokea wengi sana,rafiki yako ana kundi la ubuyu, lakini wewe sio mikato yako, kujitoa unaona kama atajiskia vibaya, unakosa cha kufanya na kuamua kuvumilia tu japo hupendi.

4)mazungumzo yasio eleweka: kila mtu anaongea lake, huyu anapiga stori na yule,huyu anamtongoza demu hapo hapo ili wengine wajue, ilihali wanaweza kufamya hivyo nje ya kundi.

5)Kukosa muongozo:kundi la vyakula watu wanapiga stori na kuulizana bei za simu, wengine wakitambiana,kukashifiana na hata kudharauliana huku kiongozi wa kundi akishindwa kumpa adhabu mwanachama kisa ni jamaa yake kafanya makosa.

Kitu gani bado? Ongezea hapo chini kwenye maoni.