Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

2.2.18

JINSI YA KUONDOA PASSWORD KATIKA FAILI LA PDF BILA PROGRAM


Karibu tena Smatskills leo tutaenda kujifunza maujanja ya kufungua na kuondoa nenosiri katika mafaili ya PDF bila ya kuwa na program maalumu za kufanya kazi hiyo kama pdf unlocker n.k
Utangulizi
Mafaili yenye Mfumo ya PDF hutumiwa sana kutuma na kusambaza nyaraka mbalimbali kwa marafiki, wafanyakazi n.k na  kubadilishana kwa usalama bila kujali mfumo wa endeshi unaotumiwa na mtumaji na mpokeaji. Mfumo wa PDF ulivumbuliwa na kampuni ya Adobe. Sasa PDF ni mfumo huru na wazi ambapo unaweza kuongeza media mbalimbali ikiwa ni pamoja na maandishi au picha, pia inawezekana kuongeza viungo vya wavuti, vitufe vya viunganishi(links) au fomu mbalimbali, sauti, video, nk. Pia unaweza kuweka saini na pia unaweza kuongeza usalama zaidi kulinda faili lako kwa kutumia nenosiri

Huenda imewahi kukutokea umepokea barua pepe yenye faili la PDF na wakati unapofungua inakuomba kuingiza nenosiri  kama unataka kuona zaidi. Ikiwa mtumaji hajakupa nenosiri  utahitaji kuwasiliana na mtumaji huyo. Kwa njia hii unaweza kufungua PDF mara chache.

Hii inaweza kuwa na ugumu ikiwa tunapaswa kuifungua mara kwa mara. Maana Itaendelea kuuliza nenosiri kila wakati unapotaka kufungua. Lakini njia hii ya leo itasaidia kuona pindi usipokumbuka au umepoteza nenosiri.
Kulinda faili la PDF wakati mwingine linaweza kuwa wazo zuri kuzuia ujumbe kuchukuliwa na watu wengine wasiokusudiwa.
Kuna baadhi ya vifaa vya uondoaji wa password katika pdf bure ambavyo vinaruhusu sisi kuondoa ulinzi password katika PDF. Hata hivyo, tunaweza pia kutumia Google chrome kuondoa nenosiri katika PDF.
Hebu angalia jinsi ya kufanya hatua kwa hatua.

Kuondoa nenosiri katika faili la PDF kwa kutumia Chrome

Kwa kuwa Google Chrome ndiyo inayotumiwa zaidi, tutaonyesha hapa chini njia rahisi ya kuondoa nenosiri kutoka kwa PDF kwa kutumia kivinjari cha Google.

 Hatua ya kwanza : bofya "Right click" kwenye faili la PDF linalodai nenosiri katika kompyuta yako. Na chagua "open with>" kisha chagua Chrome.

Hatua ya pili: kivinjari cha chrome kitakuomba kuingiza nenosiri ambalo hauna. Sasa Bofya chaguo la "Print" au uingie "Printing mode" kwa kwa njia ya kubofya "Ctrl +P" 
Sasa unaweza kufanya mabadiliko kwa kuandika jina lingine na Hifadhi kama PDF faili katika disk yako
Hatua ya tatu: Mara baada ya kuhifadhi faili lako la PDF sasa nenda kwenye sehemu iliyohifadhiwa faili lako la PDF. Kisha fungua faili la PDF kwa kubonyeza mara mbili (double-clicking)juu yake.

Hatua ya nne: Hapo sasa utakuwa umeweza kufungua hilo faili bila ya kuingiza nenosiri.


 Kumbuka: Windows 10 ina "Microsoft Print to PDF printer " ambayo imewekwa kama default. Ikiwa una toleo jingine la Windows. Ni lazima itakuonyesha wakati wa ku-print unapaswa kuchagua kuhifadhi kama PDF.

Unaweza pia kutumia vivinjari vingine kama Microsoft Edge au Mozilla Firefox na kufuata hatua sawa na nilizozielezea hapo juu kwa Google Chrome ili kuondoa nenosiri la PDF na pia unaweza kutuambia kisa ambacho umewahi kukabiliana nacho katika tatizo hili la nenosiri kwenye PDF hapo chini