Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

5.2.18

JINSI YA KUFUTA UJUMBE ULIOZIDI Dakika 7 Whatsapp .

Karibu smatskills...
 Leo tutawaonyesheni jinsi gani unaweza Kufuta Ujumbe ambao Umezidi Dakika Saba Kwenye Whatsapp.

>Kwanza Kabisa Fungua Whatsapp Yako kisha nenda Kwenye Ujumbe ambao Unataka Kuufuta kisha ukifika Angalia Tarehe Na saa Ya Ujumbe ule.

>Baada Ya kuangalia Na Ukajua ujumbe ule niwa Tarehe ngapi na saa ngapi Basi endelea na Hatua inayofuata.

>Hatua Ya Pili Ingia Settings kwenye simu yako > kisha Shuka chini na Angalia Palipo andikwa Apps manager  au kwa simu zingine pameandikwa Apps.
Bonyeza Hapo kwenye Apps manager/Apps kisha ita Load Na Kufunguka (ambapo itakuletea Orodha ya Programu zako zote shuka chini na Elekea ilipo whatsapp)
Chagua whatsapp ,bonyeza hio na Itakuleta Kwenye ukurasa mwingine ambapo utaenda Kubonyeza FORCE TO STOP.

Baada ya Kuiweka Force to stop Rudi kwenye Menu kuu ya Settings Kisha Shuka chini na Angalia ile sehemu ya   TIME&DATE .
Bonyeza Hapo kisha Itafunguka ukurasa mwingine wenye machaguo zaidi ambapo Utatakiwa kutia off sehemu zilizoonyeshwa kwenye picha hapa chini.
Baada ya kutia off sehemu hizo mbili angalia chini yake ambako awali palikuwa Pamefifia Kwa sasa patakuwa panaonekana Vizuri ambapo pameandikwa > SET DATE| SET TIME.
Kwenye SET DATE ( Bonyeza Hapo kisha weka Tarehe ya siku ambayo ulituma ule ujumbe wako kule whatsapp).

Kwenye SET TIME (Bonyeza Hapo kisha weka Mda sahihi na dakika Sahihi ambao ulituma ule ujumbe wako kule whatsapp siku zilizopita au dakika zilizopita zingatia matumizi ya PM / AM).

Baada Ya kufanya hivo Kwa usahihi TAFADHARI hatua inayofata ZIMA DATA AU WI-FI baada ya kuzima data zako basi fungua whatsapp kisha nenda kwenye ujumbe ambao ulikuwa umepanga kuufuta na Ufute kwa Kubonyeza DELETE FOR EVERYONE .

Baada Ya Hapo ujumbe utafutika kwa watu wote na hawata uona tena.
   Kisha Utarudisha Mipangilio ya Tarehe na Mda kama hapo awali kwa kuingia settings> kisha Time & Date > Automatic Time & Date na Automatic Time zone kwa kutia on sehemu hio.


TAFADHARI MAONI YAKO NI MUHIMU KWETU ILI TUJUE KAMA UMEFANIKISHA NJIA HII HIVO BASI KAMA UTAFANIKIWA TUNAOMBA URUDI KWENYE POST HII NA UANDIKE MAONI YAKO.