Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

4.2.18

HIZI NDIZO TRIKI 10 ZA TELEGRAM ZIFAHAMU SASAWatu wengi mmekuwa mnatamani kupata Triki za kufanya unapotumia Telegram basi leo smatskills tumekuletea triki hizo hapa.
      Tafadhari soma Maelekezo Vizuri na uelewe Ili uwe mjanja na wewe wa kutumia Telegram.

TRIKI 10 ZA KIJANJA KUTOKA TELEGRAM.

1 ➤JINSI YA KUBADILI MWANDIKO KATIKA SMS YAKO (BOLD) .
     Hatua za Kufuata.
Fungua sehemu ya kuandikia ujumbe(pale unapoandika ujumbe kabla ya kuutuma)
      Kisha Baada ya kuandika ujumbe kandamiza mbele ya ujumbe ambapo yatatokea maandishi haya ⇾Paste | Select All |
             Kama picha Inavoonyesha.
                   
           Kwa Hapo utabonyeza Neno Select All kisha yatatokea maandishi mengine  ambayo ni CUT |COPY |PASTE |SHARE na doti tatu mwishoni kama picha inavoonyesha.

Hapo utabonyeza kwenye Hizo doti tatu kisha utachagua Mwandiko uutakao.


2 ➤JINSI YA KUREKEBISHA UJUMBE ULIOUKOSEA (EDIT) .
            Kama umetuma ujumbe na umekosea na unahitaji Kuurekebisha Kwenye Telegram fata hatua hii > kwanza Kabisa Ingia Kwenye Chati yako kisha Tafta ujumbe ambao unataka kuufanyia marekebisho kisha Uguse Mara Moja tu yatatokea maelekezo mengi ambapo wewe utaenda palipo andikwa Edit, kisha Utabonyeza Edit hio na utarekebisha ujumbe wako kama picha inavoonyesha. 
         

       
3 ➤JINSI YA KUFICHA LAST SEEN YAKO. 
 Hii Ni kwa wale wasiopenda kuonekana wapobonline au walikuwepo online saa ngapi. 
       Kwanza kabisa Fungua Telegram Yako kisha nenda upande wa Settings (ndani ya telegram)  
          
Baada ya kubonyeza settings utapelekwa ukurasa mwingine ambapo patakuwa na mipangilio mingine zaidi shuka chini na Angalia palipo andikwa PRIVACY | SECURITY 
Baada ya kubonyeza hapo hatua inayofuata nenda palipo andikwa |LAST SEEN .
Bonyeza Hapo kisha itakuleta ukurasa mwingine ambapo utabonyeza NO BODY.  hapo tayari utakuwa Umeweza kuficha usionekane mara ya mwisho ulikuwa saa ngapi Telegram. 4 ➤JINSI YA KUFUNGIA CHATI ZAKO (LOCK) 
   Watu wengi hampendi kuonekana chati zenu kwa watu wengine hasa pale mtu anaposhika simu yako na kuanza Kukagua chati zako basi Mtandao wa Telegram umepewa uwezo huo wa kufungia chati (yaani kuzipiga Lock)  bila Kutumia Programu yoyote ile Cha Kufanya Ingia Kwenye Telegram yako kisha Fatana Nami. 
      Bonyeza Settings >kisha Privacy and security > angalia Palipo andikwa Pass code <
        

Bonyeza Kwenye Pass code kisha weka Namba ya siri ambayo utaona inakufaa kuitumia. 
Kisha Baada ya kuweka namba yako ya siri utakuwa umemaliza Kuthibitisha tu ila Huja Loki chati zako ili kuloki chati zako unatakiwa unapomaliza kuweka namba yako ya siri na kuthibitisha Rudi kwenye chati zako na Uangalie juu kabisa Utaona Alama ya Kufuli lipo wazi ambapo utabonyeza hapo kulifunga. 
Ni hivo tu. 


5 ➤JINSI YA KUBLOCK NAMBA YA MTU ASIKUPATE KABISA TELEGRAM. 
    Wengi tunafahamu kumblok mtu kwenye whatsapp na mitandao mingine ila kwa Telegram kwa baadhi ya watu kama kuna Ugumu flani hivi, haya twende pamoja. 
      Kama unataka kumblok mtu asikupate kabisa kwa telegram kwanza kabisa Fungua Chati yake wewe na yeye ambapo huwa mnachatia. 
        

   Baada ya Kufungua chati hio Angalia Juu kabisa Kisha Bonyeza Kwenye Namba Au jina Lake hapo kama mshale unavoonyesha hapo kwenye picha ↑.
     Kisha Itafunguka ukurasa Mwingine ambapo Utaangalia Juu Mkono wa kulia Kuna Vidoti vitatu kwa pembeni utavibonyeza ambapo itakuletea Machaguo chagua BLOCK.

  Ukibonyeza Block Mara Moja Utakuwa Umemaliza zoezi.

6  ➤JINSI YA KUSOMA UJUMBE ULIOTUMWA BILA KUFUNGUA TELEGRAM  YAKO(aliyetuma hata jua kama Umeusoma). 
       
Soma ujumbe bila kwenda mtandaoni
Unaweza kusoma ujumbe ambao mtu kakutumia Mda mchache kwenye Telegram bila kwenda kwenye mtandao kupitia uhakiki wa ujumbe(MESSAGE PREVIEW)  katika arifa(NOTIFICATIONS )lakini si kama ujumbe Uliotumwa mda mrefu.
     Naam, unaweza kusoma ujumbe mrefu bila kwenda mtandaoni na ni rahisi sana Fata Hatua hizi kwanza Ingia kwenye telegram yako kisha settings> kisha Notification < angalia Palipo andikwa Message Preview.
 
 


Hakikisha Notification zinakuwa Enable kisha Na Message preview inakuwa imetiwa On. 
Sasa Baada ya kuweka hivo 
Unapopokea ujumbe kwenye Telegram, zima data Au WiFi au weka Air Plane Mode |✈️ flight mode). Kisha, fungua Telegram na soma ujumbe. Baada ya kumaliza, funga programu na ufungue mtandao. Ndivyo hivo, Mtu wako hatajua kama umeona ujumbe.

7 ➤JINSI YA KUTAFTA UJUMBE WA ZAMANI.
       Kuna mda Unataka Kutafta Ujumbe wako wa zamani au wa mtu kupitia Telegram ila kutokana na Mmechati sana kiasi kwamba Jumbe ni nyingi unaona uvivu basi Triki hii hapa ya Kuupata kwanjia Nyepesi bila kuumiza Kichwa.
 Njia Hii ni inatumika Popote pale iwe ni kwenye kwenye Grupu/Binafsi au Channel.
   HATUA ZA KUFUATA.
nenda kwenye mazungumzo ya mtu binafsi au kikundi na angalia Mkono wa kulia juu pembeni kuna doti tatu bonyeza hapo kwenye hizo doti tatu na uchague "Search".

 Kisha, andika Baadhi ya maneno au maandiko unayoyakumbuka kwenye ujumbe qa zamani huo kisha Bonyeza Search. Baada ya Hapo utaletewa Jumbe Hizo papo hapo.

8 ➤JINSI YA KUIFUTILIA MBALI AKAUNTI YAKO YA TELEGRAM. 
     Kama ulishawahi  kujiuliza ni kwajinsi gani unaweza kufuta akaunti ya Telegram basi fahamu kuwa TTelegram wana namna yao ya kufuta akaunti ambayo ni tofauti Na Mitandao mingine. 
     Telegramu inajumuisha fursa ya kuharibu au kufuta akaunti yako ila Hii ni ikiwa haujatumia akaunti yako kwa muda mrefu.
Ingia Settings >-> PRIVACY |SECURITY kisha ACCOUNT  SELF DESTURCTS.


Unaweza kuweka Ni muda gani usipokuja Hewani  unataka akaunti  ifutwe.

9➤JINSI YA KUZUIA USIPATE ARIFA (NOTIFICATION KUTOKA KWENYE CHATI YOYOTE TELEGRAM).
    Mda Mwingine Unakuta unafanya jambo ambalo hupendi kusumbuliwa na Chati za Watu kwenye Telegram (zinakukela) hivo nitakuonyesha Njia ya kulitatua hilo ni Rahisi tu. 
    Fungua Telegram kisha >Ingia Settings >kisha Notification > na chagua Unataka Kuzia kwa mda gani usipate usumbufu. 
10 ➤JINSI YA KUFUTA UJUMBE ULIKOSEA KUUTUMA UKAFUTIKA NA WATU WASIUONE TENA KWENYE TELEGRAM. 
     kuna Mda Unakosea ujumbe kutuma au ujumbe ule haukuwa ni Kwaajili ya Chati ile Ila ukataka Kuifuta na ukakosa Njia basi hii hapa njia nyepesi tu.
   Kandamiza Ujumbe unaotaka kuufuta Kisha angali juu kabisa ya Chati yako utaona alama ya Dastibini ambapo utabonyeza Hapo kisha itakuuliza >Delete For Everyone >Bonyeza Hapo Kisha futa ujumbe wako .

     
Usishangae kuona Utofauti na Telegram yako hapo nimetumia (TELEGRAM X) ila Kila kitu kipo sawa hata kwenye Telegram ya zamani .
TELEGRAM X nitoleo Jipya kabisa kutoka Telegram


PIA SOMA :  SIRI USIZOZIFAHAMU USIZOZIFAHAMU KUHUSU TELEGRAM.

  Basi hizo Ndizo triki kumi za kutumia Telegram bila kupata shida.

Maoni usaidizi Ruksa kutolewa.