Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

4.2.18

HII NDIZO SIRI MBILI USIZOZIFAHAMU KUHUSU TELEGRAM.

Telegram Ni mtandao wa kijamii ambao unakuja kwa kasi Hivi karibuni na Kuwa na Ubora zaidi kuliko mitandao yote ya kijamii sema Hauna watumiaji wengi sana Duniani ila ni mmoja kati ya mitandao Bora kabisa. 

Telegramu ilianzishwa na mjasiriamali wa Kirusi Pavel Durov.
Mnamo Februari 2016, Telegram ilieleza kuwa ilikuwa na watumiaji milioni 100 kila mwezi, na watu kutuma ujumbe bilioni 15 kwa siku. Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wake, mnamo mwezi wa Aprili 2017, Telegram ilikuwa na kiwango cha ukuaji wa mwaka zaidi ya 50% na inakuja kwa kasi.
KUNA VITU KATIKA TELEGRAM AMBAVYO KIUKWELI WENGI HAWAVIJUI NAKAMA WANAVIJUA BASI HAWAVIELEWI.
   Ndio maana Leo smatskills tumeandaa makala Ambayo Itakufanya kauifahamu Telegram kwa undani zaidi na Features zake.

HII NDIO MIPANGILIO YA SIRI YA TELEGRAM IFAHAMU HAPA.

1 :SECRET CHAT. 
  Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa telegram nadhani umeshaona hii sehemu ambayo inaitwa secret chart.

     > Secret chat ⇾nini maana Ya Hii kitu hii??
secret chat ni kwamba utaweza kuanzisha Chat ya siri wewe  na Mtu ambaye umeanzisha chati nae ya siri (Tumia Hii ikiwa mtu unayechati nae ni mtoa siri au humuamini kabisa ) Yaani kwenye chati hiyo ya siri unapoianzisha na Mtu wako Mambo yafuatayo hatoweza Kuyafanya pia na wewe huwezi kuyafanya.
 >Hutoweza kupiga screen shot yale maongezi. 

 >Hutoweza kufowadi hayo maongezi kwa mtu mwingine. 

> Hutoweza kunakili maongezi hayo na kuyatuma kwa mtu mwingine. 
  ⇢Yaani kila mtakacho chati kitabakia pale pale hakitatoka nje ya Telegram (kwenye chati yenu)  na ndio maana ya Secret chat.

Jinsi ya kuweka SCRET CHAT.
   Fungua Telegram yako kisha Nenda kwenye chati yako wewe na mtu wako , bonyeza kwa juu palipo jina lake au namba yake (mfano picha inavoonyesha)
Kisha itakupeleka kwenye ukurasa mwingine ambapo utabonyeza Doti datu zilizoko mkono wa Kulia pembeni (mfano picha inavyoonyesha) 
Baada ya kubonyeza kwenye doti hapo yatatokea machaguo mengi chagua secret chat( mfano picha inavoonyesha) 
Baada ya kubonyeza hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye Secret chat ambayo uliyeanzisha naye secret chat akiwa Yupo online kwa mda huo atapokea Taarifa ila kama Yupo offline utasubili mpaka aje online.

 Set self-destruct timer in Secret chats


Nini maana ya Hio kitu?? 

Hii maana yake ni kwamba Weka mda wa kuharibu /kufutilia mbali ujumbe ambao umeutuma kwenye mazungumzo ya Siri(Secret chat). "Mazungumzo ya Siri" ya Telegramu ni kipengele maarufu kabisa, kwa sababu huleta ufikiaji wa mwisho hadi mwisho, arifa za skrini pamoja na vipengele vingine vya usalama. 
Lakini kile tunachopenda zaidi ni uwezo wa kuweka mda wa uharibifu kwa ujumbe uliotumwa kwenye mazungumzo ya siri. 

Ili kuweka timer, Bonyeza Sehemu yenye doti tatu kwenye mazungumzo ya siri na Bonyeza  "set self desturcts timer". Kisha, chagua mda ambao maana yake ni kwamba kila Ujumbe utakao tuna au kutumiwa Utaftika Automatiki kwenye Mda uliouchagua. 

2: PLAY VIDEO IN ANOTHER WINDOW ON TELEGRAM. 
Katika Telegram kuna Mambo mengi mazuri hili nalo ni mojawapo( jinsi gani unaweza kutazama video kwenye Telegram huku ukiendelea kuchati). 
Hii ni Moja Ya Mambo ya Siri sana kwenye Telegram ila smatskills Tumekufunulia Siri hii. 
Fungua video unayotaka Kuitazama Uliyotumiwa huko Telegram iwe ni kwenye Grupu au Chati binafsi . >kisha Play video hio. (Mfano picha inavyoonyesha) 
Baada Ya kuipata video yako basi Play video hio. 
Kisha ikiwa ina play vile angali alama ya kijidirisha ambacho kipo juu mkono wa kulia. (Kama picha inavyoonyesha) 
Bonyeza Kialama hicho automatiki itatoka hao na utaanza Kuitazama video huku ukiwa una chati na watu wako. 
Video itakaa kama hivi 👇(picha hapo chini) 

Na utakuwa una chati huku unatazama video. 
Nadhani umeweza Kutanbua siri hizo je 
Una Maoni ushauri??  Tuandikie Kupitia sanduku letu la Maoni.