Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

20.2.18

APPS MUHIMU ZILIZOKOSA UPENDEZI KWA WATUMIAJI

  Kila kampuni ya simu ina apps tumizi zake ambazo lazma zije na simi,pamoja na nyingine kuwa ndani ya simu[kwenye system]mara nyingi apps hizi hazipendwi sana na watumiaji kwahiyo huonekana kama haina manufaa. Ngoja tuone baadhi ya apps hizo.


SOMA PIA: APPS KUMI MUHIMU KWENYE SIMU YAKO

  1.Palmchat,chat:-hizo apps za kupiga soga kama zilivyo WhatsApp au Facebook, palmchat huja na tecno na itel lakini zimeshindwa kutoboa kwenye soko kutokana na ushindani kuwa mkali, vivyo hovyo kwa chat ambayo ni maarufu kwa Samsung,lakini badala ya kupendwa ndio kwanza imelalamikiwa na watumiaji wa simu hizo, kwa kuwa wameiona haina kazi na inakuja na kila Samsung.

 2.Calcare:- hii inakuja na simu za Tecno, itel,infinix na baadhi ya simu nyingi toka China,kazi ya hii app ni kujua sehemu unakoweza kupata huduma pale simu yako itakapopata tatizo,yani ina mawasiliano ya matawi yote, na ramani ya matawi hayo yalipo, kwahio kama simu yako ina tatizo fulani na upo labda Tanga, ukiingia calcare unaweza kujua ni wapi naweza kutengenezewa simu yangu.

 3.Accuweather:- kila simu sasa inahudumiwa na hii app kwenye mambo ya hali ya hewa, wengi wameikuta kwenye simu zao na kutokana na ipo kwenye system basi haiwezi kutoka, lakini wengi hawana matumizi nayo pamoja na umuhimu wake, unaweza kujua hali ya hewa kwa siku hiyo, kesho n.k,unaweza kuweka widget ya miji unayotaka ikuoneshe hali ya hewa ya sehemu hizo.

 4.Backup:- hili ni tendo la kuokoa data za simu yako hasa unapofuta kila kitu(restore) au kuuza na kununua simu ingine, kuna njia na aina nyingi za kubackup.
  • Njia:- barua pepe,hifadhi ya kumbukumbu sim kadi yako au hifadhi mbali mbali za mtandaoni kama goole drive, mediafire na dropbox
  • Aina:-kila kitu kwenye simu yako ni muhimu,lakini kuna vile ambavo ukishafuta simu yako havirudi tena kama majina, jumbe, apps tumizi, faili mbali mbali kama pdf n.k.


 5.Barua pepe:- hii ni tofauti na app ya Gmail, ipo kils simu, hata kwa visimu vya zamani kama nokia huduma hii ilikuepo, watu wamekuwa wakiipotezea kutokana na urahisi wa kutumia Gmail,app hii ya barua pepe hii haichagui kampuni ya kutuoa huduma kama ilivyo kwa gmail, hii unaweza kujaza barua pepe yeyote na kuona barua pepe zako.

Apps zingine
Tecno spot[forum ya tecno]
Xclub[forum ya Infinix]
Hicare[huduma kwa wateja Huawei/honol]
Zipo nyingi kulingana na simu.

Kama kuna neno nimekuchanganya hujaelewa liandike kwenye maoni chini na mm nitakutajia, mf barua pepe=email.