Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

5.1.18

UTAFANYA NINI KAMA SIMU YAKO IMEANGUKIA KWENYE MAJI???? SOMA HAPA SOLUTIONS YAKE!!!!


HATUA ZA KUFUATA:

1:Kwanza Kabisa unatakiwa kuizima ,Kama ilikuwa Tayari ishazima Utatakiwa kufanya hivi iinamishe mkono wa kulia juu.

2:Kama simu yako ina Cover Itolea Mara moja Kisha Toa mfuniko ,pia Kama Simu yako sd cards, Sim card(line) vipo kwa nje toa na vyenyewe Mara moja.


3:Fungua Kwa nyuma na Toa mfuniko Na kama Sd Card na Line vipo kwa Huko Navyo Toa kwa mda huo.

4:Tumia Nguo, kitambaa Au pamba kavu kufuta sehemu zilizo na maji maji kwa Hapo panapoonekana pameloa.
   Kumbuka hakikisha Batter, line au Memory card viko nje kwa mda huo.

Kama Maji yamezidi sana yaani yameingia kwa ndani zaidi fata hatua hizi hapa chini:

  1:Chukua kibegi kidogo Kijazie Mchele Wa kutosha Kisha chukua smartphone yako iweke Humo kisha funga Begi lako na Tunza mahala pakavu na penye usalama.


2:Iache kwa mda wa Siku moja au Mbili zipite.

3:Usijaribu kuiwasha Kabla ya Siku hizo kufika au kuisha.

4:Kuwa mvumilivu kwa siku hizo chache Tumia simu ya ndugu au jamaa Kwa siku hizo mbili tatu.


  BAADA YA SIKU HIZO KUISHA AU KUFIKA:

weka Betri Kwenye simu na kisha washa Simu yako, kama Simu haitowaka jaribu kuiweka chaji, kama Isipopeleka chaji au kuwaka Basi Betri itakuwa Imeathirika hivo Badili Betri.

Pia Kama ukiwa umebadili Betri na bado Haikuwaka Tafadhari ipeleke kwa Mtaalamu ikaangaliwe vizuri.

   Hizo ndio njia Za awali za Kuifanyia simu ambayo imepata athari ya Maji.

 Muhimu: Kumbuka Inapoangaukia Kwenye Maji vitu ambavyo hutakiwi kuvifanya.

   >Hutakiwi kuiwasha
   >Hutakiwi kubonyeza Botton yoyote ile iwe ni zile za Kuongezea sauti au Ya kuwashia simu.
  >Hutakiwi Kuitingisha (utasababisha maji kusambaa zaidi)
 >Hutakiwi kuibonyeza Bonyeza kioo, kuizungusha zungusha Pia Hutakiwi.

   KAMA SIMU YAKO BETRI LAKE SIO LA KUTOA:
 >Unatakiwa ile sehemu ya kuingia Earphones simu uiinamishe Chini yaani maji utayaelekezea sehemu hio.

>Usiiwashe Iache tu!
>kama unavifaa vya kufungulia ifungue ila hakikisha unaifungua kwa uangalifu zaidi maji yasielekee sehemu ya kioo.


    Kwa kufanya Hivo utaokoa Gharama za Kununua simu Mpya. Na utakua Umeokoa simu yako hio.