Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

10.1.18

Toleo jipya La Whatsapp Hivi Karibuni Waongeza Vipengelee zaidi vizuri!!!

Whatsapp Wapo katika Majaribio ya mwisho kwa ajili ya kuachia Toleo jipya hivi karibuni.

   Sasisho hilo la WhatsApp linaonyesha vipengele vipya vilivyowekwa Ni Vipengele muhimu sana na vizuri kwa mtumiaji ambapo itakuwa bora kwa watumiaji wa Mtandao wa Whatsapp Ambapo Toleo la sasisho hilo litakuwa ni Android version 2.17.443.


MAPYA NA VIPENGELE HIVYO KATIKA TOLEO HILO:

1:> Group Administration (Admin)  Sasa Ataweza Kufuta ujumbe wa Member wa kawaida

2:>Video Calls Kwa Magrupu Sasa imewezeshwa.
3:>Voice calls Kwa Magrupu pia imewezeshwa.
               
Ufafanuzi Kuhusu kipengele cha pili na Tatu:
  Hapo itakuwa hivi member Yeyote ataweza Kupiga simu kwa Njia ya Video au ya sauti Katika Grupu Husika ambapo yumo na member wengine wataweza kuipokea simu hio na kusikiliza simu hiyo iliyopigwa.  Tofauti na hivi sasa ambapo utapiga simu kwa njia ya video au sauti kwa mtu mmoja!!4:>Stika za Facebook sasa utaweza kuzitumia Kwenye toleo hilo jipya La Whatsapp.
   
5:>Private Reply (Group)
 Hii ipo hivi Mfano member mmoja katuma ujumbe katika Grupu na Ukataka kuujibu ukumbe ule kuna machaguo mawaili Kuna Kujibu ujumbe ule na Member wote wakaona ulivyo jibu Au ukajibu ujumbe ule na Mhusika wa ujumbe ule Akaona yeye tu ndio maana ya (Reply private).

Whatsapp Hawajabainisha Tarehe wa ni lini toleo hilo litatoka Japo lipo mwishoni katika majaribio yao.

Kaa nasi Tutakujuza zaidi

smatskills ©2018.