Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

18.1.18

OPPO A83 simu yenye teknolojia kama Huawei Mate 10

  Oppo ni moja ya kampuni ya simu janja inayokuja kwa kasi sana, hadi inatishia soko la wakongwe.
 Safari hii wamezindua Oppo A83 yenye teknolojia kama simu ya Huawei Mate 10 ambayo ni Artficial Intelligence.

SOMA PIA: Ijue tofauti kati ya MB na Mb

    ARTFICIAL INTELLIGENCE NI NINI?

Hii ni teknolojia ndani ya vifaa vya kielekitroniki, hii inafanya mashine iweze kukisia na kutambua kitu kwa urahisi, yani unaweza kupiga picha kitu au vitu na kupitia hii ukajulishwa hii ni picha ya kitu gani,ni mengi sana kuhusu teknolojia hii.

  Huawei Mate 10 ndio iliyotangulia kuja na huduma hii kwa upande wa simu janja, lakini tunaona Oppo wananyemelea kwa kasi sana.
              Baadhi ya sifa za Oppo A83
  • Mfumo endeshi OS android 7.1 Nougat
  • Kamera ya mbele 8 MP
  • Kamera ya nyuma 13MP
  • Kioo: 7-inch HD+ (1440 x 720) LCD 
  • Diski uhifadhi 32GB[ikiwa na sehemu ya memori mchomeko hadi 256GB]
  • Ram 3GB
  • Prosesa ni MTK6763T
  • Betri 3180 mAh


Simu hii inakadiriwa kuwa $220 ambayo kwa shilingi ya Tanzania itakuwa ni Tsh 493,000 kulingana na viwango vya sarafu kwa siku hiyo.

  Unaionaje hii simu, ikifika Tanzania utanunua?