Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

30.1.18

MOBIUS 2 Gari ya kwanza kutengenezwa Kenya

 Afrika  inazidi kupiga hatua kiteknolojia, wiki kadhaa Misri ilitengeneza simu aina ya Nile X, Uganda nao wanajiandaa kurutubisha nyuklia na  wametengemeza mabasi yanayotumia umeme wa jua,hapa TZ nako TTCL wametangaza kuanza kutengeneza simu pia,yote hayo ni maemdeleo.

Soma pia: Nile X simu janja ya kwanza kutengenezwa Afrika

  Kenya wamezindua gari aina ya Mobius 2 iliyotengenezwa maalumu kwa barabara za Kiafrika,yani inaweza kutumiwa popote,kwenye changarawe na lami pia, gari hii ni kubwa na ina nguvu sana bei yake ndi ndogo kulinganishwa na magari mengine,bei inayoendana na mahitaji ya Kiafrika pia.
Muonekano wa picha za Mobius 2 na jinsi ilivyotengenezwa
Bei ya gari hii inakadiriwa kuwa ni Milioni 28 za kitanzania,ni tofauti kabisa na gari aina nyingine za mfumo huo,ambazo bei iko juu.

Soma pia:Acer Swift 7 Laptop nyembamba kuliko zote duniani kuingia sokoni april 2018

Kenya ni mfano wa kuigwa na nchi zingine Afrika Mashariki kwa hatua yake.

Hii gari unaonaje? Italeta ushindani mkubwa sokoni au kawaida tu? Nipe maoni yako chini hapo.