Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

4.1.18

Mamia ya programu za smartphone hufatilia watumiaji wake kupitia Microphone

Je unafahamu kuwa Kuna Mamia Ya Apps na Games humfatilia Mtumiaji wake kwa njia Ya Microphone???
   

Software kutoka kwa kampuni inayoitwa Alphonso ambayo imeweza kutumika kusikiliza katika mazingira karibu na mtumiaji, kufanya kazi nje ya kile wanachokiangalia Ni moja kati ya program zinazofatilia Watumiaji wake kwa njia ya Microphone.
         

Wao hujumuisha teknolojia hii ambayo inaweza hata kutambua Kitu wakati mtumiaji anaweka simu yake ndani ya mfuko, ikiwa kama programu inafanya kazi Background.

Programu hizi, ambazo  zinazolengwa kuwa ni Moja kati ya njia za kufanya utafti kiteknolojia zaidi ,unapo tumia programu kutoka Alphonso ambayo hukusanya kimya data zake kuhusu tabia za watu kutazama TV  na kuziuza kwa watangazaji kwa matokeo zaidi.

Karibia Games  1,000 na programu za jamii zimehesabiwa kutumia programu hiyo ya Alphonso , na zaidi ya 250 kati ya hizo zinapatikana na kupakuliwa kutoka Google Play store na idadi ndogo pia inapatikana kutoka kwenye Duka la App Store la Apple.

Wakati huu kampuni ya Alphonso bado haijajulisha majina ya programu hizo pamoja na Games ila zinazo dhaniwa ni
Pool 3D, Beer Pong: Trickshot, Real Bowling Strike 10 Pin na Honey Quest.

Kampuni hiyo inasisitiza kwamba teknolojia yake hai Rekodi wala kutunza kumbukumbu ya mazungumzo ya watu bali inatafta takwimu kuhusu vipindi Mbali mbali katika Runinga, na inasema uwezo wake umeelezwa wazi katika maelezo ya programu na sera za faragha.(privacy &policies)


Descriptions (maelezo ) ya Game la Poor 3D, "Programu hii imeunganishwa na programu ya Alphonso Automated Content Recognition (" ACR ") iliyotolewa na Alphonso, (third party service) huduma ya tatu> unapo fungua Game hilo litaomba Permission (Ruhusa) ya Microphone Kama moja wapo ya Permission zingine, Na Baadae programu ya ACR inapata sampuli za muda mfupi za sauti kutoka kwenye Microphone kutoka kwenye kifaa chako. "

"Ikiwa mechi inapatikana, Alphonso inaweza kutumia taarifa hiyo kutoa matangazo muhimu zaidi kwa kifaa chako cha mkononi. Programu ya ACR inanasa maudhui yanayojulikana ya sauti na haijui au kuelewa mazungumzo ya binadamu au sauti nyingine. "

Ashish Chordia, mtendaji mkuu wa Alphonso, aliiambia New York Times kwamba Alphonso imefanya kazi na studio za filamu, ambayo hutoa ushirikiano kwa kampuni kabla ya kutolewa kwa filamu, na iwe rahisi kwa programu kutambua.

      Smatskills©2018.