Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

13.1.18

Je Simu yako Inaishiwa Chaji haraka hata kama hutumii simu kwa mda huo???Je Betri ya simu yako huishiwa chaji haraka Au Unapoweka simu chaji inapeleka polepole???
   Smatskills Tupo hapa kukusaidia Kulitatua hili tatizo Na tatizo hili Linawakuta watumiaji wengi wa simu janja na Wengi wao hawajui nini cha kufanya.

Basi tutazame kisababishi cha Tatizo hilo Na Njia ya kutatua tatizo hilo.

Kisababishi kikuu : programu-hogging (Apps Na games Kushindwa Kuitikia wito)
programu ni baadhi tu ya matatizo ya simu za Android kuwa na utendaji mbaya wa betri. Lakini tuko hapa kusaidia.
Kuna baadhi ya program zinashindwa kufuata kile unachokihitaji unakuta umemaliza kuitumia lakini ukaifunga Kabisa ila baadae ikaanza kujiendesha yenyewe na hivo unaweza kukuta zinafanya kazi background bila wewe kuwa na taarifa hivo chaji itatembea haraka zaidi kuliko kawaida.
 
           Jambo la muhimu ni kwamba- Tunahitaji kujifunza tabia ya betri zetu ili kupata tatizo na hatimaye kupata suluhisho. Ili kupata uelewa bora wa nini kinachofanya betri yako iishi, nenda kwenye Mipangilio> Battery.

Vilevile kuna Program Zingine zinakula sana Moto bila wewe kujua Na Hata kama haifanyi kazi Background Yaani yenyewe kwa jinsi ilivo inamaliza Chaji.

 AVG Company Walitoa Ripoti ambayo inaonyesha programu ambazo zinakimbiza betri zaidi - huenda unaendesha baadhi ya program hizo  kwenye simu yako.
   Ripoti Hio itakujia Hivi karibuni endelea kuwa nasi smatskills Ila baadhi ya Program hizo ni pamoja Na Facebook, snapchat & BBC News.

Ikiwa unataka kwenda kwa undani zaidi kuhusu matumizi ya betri ya smartphone yako, utapata programu kadhaa kwenye Hifadhi ya Google Play ambazo hutoa takwimu na maelezo ya kina juu ya matumizi ya betri. Tunapendekeza tumia Program ya Monitor GSam Battery.

Mara baada ya programu imewekwa, inachukua siku kadhaa kukusanya data kwenye matumizi yako ya smartphone na betri, halafu baada ya hapo itakupa maelezo mafupi juu ya nini unatumia betri gani kwenye kifaa chako.

hio ndio sababu  inayosababisha betri au simu kuwahi kumaliza chaji haraka. 

NJIA YA KUZUIA HILI LISIKUSUMBUE :

Na kama unatatizo hilo la apps Kutumika Background Bila wewe kuwa na Taarifa Basi tatizo hili litakusumbua sana unapaswa kutumia program za kuzuia jambo hili lisiendelee kukusumbua, kuna baadhi ya program Za kuzuia jambo hilo ila Tunapendekeza Tumia ADVANCED TASK MANAGER
Advanced Task manager Inakata Apps zote zina run Background Na Kuzizuia Kupelekea Chaji haraka Ijaribu leo. 

SIMU YAKO INAPELEKA CHAJI POLEPOLE???? 
Fahamu hapa Visababishi ambayo Vinachangia kwa kiasi kikubwa Tatizo hilo. 

1:Kuchangia Chaja
2:Betri Ya simu kuwa imechoka

>Kuchangia Chaja  kuna Baadhi ya Simu ukichangia chaja Tatizo la Kupeleka chaji linapungua kwa kasi sana Na hii wengi inawakumba bila wao kufahamu Hivo unashauriwa Kuchangia Chaja kwenye simu inayoendana Na yako Yaani kama ni Samsung kwa Samsung Nasio Chaja ya Samsung ukachangia kwa Tecno. 
Hio Itasababisha Simu kupeleka chaji Taratibu. 

2:Betri Ya simu kuwa imechoka
Hapa Ni kutokana na mda wa betri yako tangu uinunue Kama ina mda Mrefu umeinunua Fahamu ya kwamba inaenda inapoteza Uwezo hivo huwa inashindwa kupokea Chaji kama Hapo Awali.

hivo Ukiona Chaji inapeleka Taratibu Chunguza kwa makini Eidha Ni Hayo Mambo yanasababisha .

Smatskills ©2018