Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

12.1.18

Ijue tofauti iliyopo kati ya MB na Mb

Kushindwa kutofautisha kati ya Mb na MB limekuwa ni jambo linalowachanganya watu wengi tu bila ya wao kujua sasa leo tutaondoa utata huo
Utangulizi
MB ni nini?
MB ni kifupisho cha maneno ya kiingereza Megabyte ambacho ni kipimo kinachotumika kuonyesha ukubwa au kiasi cha data/file mfano movie inaweza ina MB 600
Na pia vile vifurushi cha data  unavyopewa na mtoa huduma wako wa internet (ISP) pale unapojiunga hizo nazo pia ni MB japo kuna vizio vingine vinavyotumika kuonyesha ukubwa wa data kama KB,GB,TB n.k ila MB imezoeleka sana kutumika

      

Kwahiyo pale unaponunua kifurushi kwenye mtandao wako huwa unapata MB na wala sio Mb kama watu wanavyochanganya

Mb ni nini?
Mb ni ufupisho wa neno la kiingereza  Megabit ambalo hutukimika kama kipimo kuonyesha kasi ya usafirishaji wa data kutoka kifaa kimoja kwenda kingine
Mfano kurusha mafile kutoka kwenye simu moja kwenda nyingine au kutoka kwenye simu kuenda kwenye kompyuta n.k
Internet  pia hutumia hiki kipimo kuonyesha speed ya kupakia na kupakua mafile kwenye mtandao
Mfano mtandao unaotumia
Unaweza kuwa na kasi ya 2Mb/s au 2Mbps ikiwa na maana megabit  mbili kwa sekunde au 500kb/s ikimaanisha speed ya internet yako ni kilobit 500 kwa sekunde

Kitu kimoja ambacho huwapa watu mkanganyiko ni kutofautisha kati ya Megabyte (hutumika kwa ukubwa wa faili) na Megabit (hutumika kwa kasi ya kupakua/kupakia). Watu mara nyingi watu hudhani kuwa kasi ya kupakua 1 Megabit kwa sekunde (1 Mbps) itawawezesha kushusha faili ya Megabyte moja kwa sekunde. Hii sio kweli, Megabit ni 1/8 kwa Megabyte, inamaanisha kwamba kupakua faili la MB 1 kwa sekunde unahitaji kuwa na internet yenye kasi ya 8 Megabit kwa sekunde(8Mbps). pia tofauti kati ya Gigabyte (GB) na Gigabit (Gb) ni sawa na ilivyo kwa Mb na MB, Gigabyte ni mara 8 kubwa kuliko Gigabit.

Mbps inamaanisha megabits kwa sekunde. Ambayo hutumiwa kuonyesha kasi ya kupakua na kupakia mafile(Download and upload speed).

MBps inamaanisha megabytes kwa sekunde. MB hutumiwa kuonyesha ukubwa wa faili.

Soma pia:NILE X SIMU JANJA YA KWANZA KUTENGENEZWA AFRIKA

Utakuwa umekutana na maneno haya unapopakua mafaili kutoka kwenye mtandao au kuhamisha data kutoka kifaa kimoja hadi kingine mfano kwa kushare mafile kwa njia ya bluetooth au wifi .Wanaonyesha kiwango cha uhamisho wa data. kasi yako ya(kupakua na kupakia) itaonyesha kama megabits kwa sekunde(Mbps). Lakini, unakuwa unapakua au kuhamisha megabytes(MB).