Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

26.1.18

IFAHAMU PROGRAMU ENDESHI YA ANDROID

 Watu wengi zama hizi wanatumia simu janja, sokoni ushindani mkali uliopo ni  kati ya programu endeshi ya iphone[iOS]  na android OS, leo tuone android ni nini? Na historia yake.

          ANDROID NI NINI?
Android ni programu endeshi inayotumika kwenye simu janja, tabiti[Tablet], saa za kijanja[smart watch] na hata tv pia, mfumo huu ni huru au huria (open source) kwa maana kwamba kama una ujuzi unaweza kuongezea ufundi wako na kuweka sokoni.

 Wamiliki na waanzilishi wa mfumo ni ni Google, kwahiyo wao ni wanaotengeneza na kusambaza kwa makampuni tofauti wanaotengeneza simu kama Samsung, LG, Sony, Tecno, Huawei Pixel n.k. Hii haimaanishi kuwa Google ni wasimamizi wa hizo simu, kazi ya Google ni kuunda hiyo programu na kuitoa kwao.

 TECNO NA SAMSUNG ZOTE ANDROID KWANINI ZINA MIONEKANO TOFAUTI?


HISTORIA YA MITANDAO YA KIJAMII!


 Google wao hutoa toleo lao linafahamika akama AOSP[Android Open Source Project] ambalo kimuonekano haina mambo mengi sana(hilo ndio toleo orijino la android) kama matoleo ambayo yamehaririwa na makampuni na kujaza apps tumizi zao,
  AOSP  ikishatoka inasambazwa kwenda kwenye makampuni mojawapo tajwa juu wao sasa wanabadilisha muonekano na kuweka wanavyotaka wao ndio zinatokea tofauti na kukuta kama hivi
  •  Samsung=>TouchWiz
  •  Huawei=>Emui
  • Tecno=>HiOS
  • Xiaomi=>Miui
Hayo ni moja wapo ya matoleo ya Android yaliyofanyiwa marekebisho na makampuni hayo,ni mengi kutokana na kampuni.

LEO KATIKA HUSTORIA JE WAJUA?


 Mpaka hapo umeelewa tofauti iliyopo kwanini simu zote ni Android lakini zina mionekano tofauti?katika makala ijayo tutaona mtiririko wa matoleo yote ya Android hadi kufikia 8[Oreo]

unapenda kupata habari mapema zaidi? karibu telegram kwenye channel yetu hii smatskillstz