Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

17.1.18

HIFADHI JUMBE NA SIMU ZAKO UNAPOBADILISHA SIMU MPYA

  Maisha yanazidi kurahisishwa kila kunapokucha, hii inayokana na changamoto za kila mara, ulishawahi kufikiria siku unapouza simu yako jumbe[massages] na simu[call logs] unaweza kufanyaje ili zihamie kwenye simu yako mpya.?

Soma pia: WhatsApp yaja na vipengele vizuri zaidi

  App maarufu inayojulikana kwa kutoa huduma ya kutambua nambari za wapiga simu sasa imepiga hatua na kufanya jambo la maana na muhimu sana, ukiwa na app hii ondoa shaka kwenye uhifadhi wa jumbe na simu zako.

  Truecaller imeona changamoto hizi na kuzifanyia kazi na sasa kufanya iwe rahisi kuhifadhi data zako mtandaoni, truecaller sio app mpya wala geni kwa watu. Kama bado hauna hii hapa

  Kinachomaanishwa sasa ukiuza simu labda Tecno na umeamua kununua Samsung kama ulibackup data zako kwa truecaller basi utapata jumbe zako zote na simu zako.
Hapo unaweza kuchagua kuhifadhi kwa siku, wiki na hata mwezi, hakikisha unaweka barua pepe [email] yako kwa ajili ya kazi hiyo.

Hiyo huduma unaonaionaje?? Niandikie kwenye maoni hapo chini, usisahau kushiriki na wenzako maujanja kama haya.