Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

17.1.18

Acer Swift 7 Laptop nyembamba kuliko zote duniani kuingia sokoni april 2018Kampuni ya kompyuta ya Acer yauanza mwaka 2018 kivingine kwa kutambulisha laptop yake mpya ya Acer Swift 7 (SF714-51)


Acer wameionyesha laptop hiyo kwenye onyesho la watumiaji wa vifaa vya kieletronic/Consumer Electronic Show(CES 2018) lililofanyika Las vegas marekani january mwaka huu

Laptop hiyo inayosemekana kuwa ndio laptop nyembamba kuliko laptop zote duniani kwasasa ikiwa na unene wa 8.98mm sawa na sentimita 0.898 hiyo ni kwa mujibu wa watengenezaji wa laptop hiyo


Ingawa Acer Swift 7 ni laptop nyembamba zaidi ila inakuja ikiwa na processor bora kabisa ya 7th-gen pia ikiwa na uwezo mkubwa wa internet ambapo imetengenezwa ikiwa na kiunganishi cha WiFi kinacho tumia teknolojia ya 4G LTE.

Laptop hii inatarajiwa kuingia sokoni rasmi kuanzia mwezi wa nne (Aprili) mwaka huu ikiwa na bei ya dollar za kimarekani 1,699 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 3,900,000.
Sifa na Uwezo wa Acer swift 7(SF714-51)
📌Aina ya Processor; 7th-generation Intel Core i7 processor
📌Ukubwa RAM; 8GB LPDDR3 memory
📌 Ukubwa wa Kioo; Kioo kina ukubwa wa inch 14 kilicho tengenezwa kwa Corning Gorilla Glass pia kina uwezo wa touchscreen kikiwa na resolution ya 1,920×1,080-pixel
📌Keyboard;  Keyboard yake inawaka taa au Backlit keyboard
📌Mfumo wa Uendeshaji(OS); Inatumia Windows 10
📌Ulinzi; password kama kawaida ila ina sehemu ya alama za vidole (fingerprint reader)
📌Battery; Inakaa mpaka Masaa 10 na chaji ikiwa imejaa
📌Ukubwa wa uhifadhi (Hard Disk/SSD);Ina 256GB SSD storage yenye teknolojia ya PCIe

Kwa habari zaidi za masuala ya teknolojia na maujanja mbalimbali hakikisha una download App yetu mpya ya Smatskills na vilevile tembelea
channel yetu ya Youtube Smatskills ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.
Pia usisahau kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii ili kupata taarifa kwa haraka kila tunapoweka habari mpya mtandaoni