Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

7.12.17

Kaa tayari kwa ujio wa Messenger kids

Hii ni huduma mpya toka Facebook ambayo ni maalumu kwa watoto.

Muonekano wa Messenger kids 


Messenger Kids inatarajiwa kuwapa watoto ufahamu kuhusu nembo ya Facebook na hivyo kuongeza uwezekano wao kusalia kwenye mtandao huo. Facebook wamechukua hatua hiyo huku wakiendelea kupata ushindani mkali kutoka kwa Snapchat.

Mtoto akiwa na Messenger kids anaweza kuwasiliana na kutafuta marafiki wenzake kwa njia ujumbe mfupi video na mtoto mwenzake ila tu kwa idhini ya wazazi.
Toleo hili limelenga watoto chini ya miaka 13 hadi 6 na kwa sasa linapatikana katika vifaa vya iOS na adroid kwa Marekani tu.

Unasubiri toleo hili kwa hamu?? Niandike kwenye uwanja wa comment chini hapo
      Chanzo BBC