Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

16.12.17

JINSI YA KUFANYA DREAM LEAGUE KUWA GUMU

  Ukitaja michezo (games) maarufu ya  mpira kwenye  simu basi hutakosa kujua Dream league.
 Ni moja ya mchezo ambao umeandaliwa vizuri sana.
 BAADHI YA SIFA ZA MCHEZO HUU

  •  muonekano wake[3D]
  •  ‎uchezaji wake 
  •  ‎kucheza wawili (wewe na rafikiyo) 
  •  ‎kucheza mtandaoni(online) na mdau mwingine
  •  ‎na cha kuvutia zaidi ni pale unapocheza offline(bila kuwasha data).
SOMA PIA
PES 2018 MODS FTS 18 IN ONE GAME ;PAKUA HAPA NA JIFUNZE JINSI YA KUINSTALL

HACK DREAM LEAGUE SOCCER 2018


 ‎   Baada ya wajuzi kulizoea sasa wamehangaika sana jinsi gani wanaweza kulifanya liwe gumu kucheza.
 ‎
Funga magoli makali

 ‎FANYA HIVI UFURAHIE UPINZANI WA KWELI:

Huenda ushachukua vikombe vyote kwenye mchezo huu na magoli mengi tu,na sasa unaona mchezo wako sio mgumu tena na hata umeanza kuuchukia, sasa soma makala hii kwa makini.

HATUA YA KWANZA :
Uza wachezaji wote mastaa wote kwenye timu,kwanini ni muhimu???
Hii itapelekea mastaa hao kwenda kusaidia timu zao za zamani na hivyo kila kikosi kitakuwa na nguvu.

HATUA YA PILI:
Sajili wachezaji wa kawaida sana hata kama wana majina lakini watoke timu ndogo za daraja la chini, ili uwakuze wewe na kupata upinzani toka kwa mastaa wa timu kubwa.
Hakikisha unaongoza kila kitu sio ushindi tu


HATUA YA TATU:
Usicheze mchezo ili ushinde tu, unaweza kufurahia mchezo kwa kupiga pasi nyingi kupiga  chenga,kuangalia je umeongoza kwenye umiliki wa mpira kwa asilimia ngapi? na manjonjo kibao kabla ya kufunga, au hata unaweza kupiga goli katikati ya uwanja, au hata kufunga kona moja kwa moja.
Una swali niandikie chini hapo na utajibiwa kwa ufuasaha, kama unatumia telegram karibu kwenye kundi letu SmatSkills

Jaribu kufanya hivyo afu niambie unaonaje.