Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

25.12.17

APPS 6 BORA KWA MWAKA 2017 !! TAZAMA HAPA!


Karibu mpendwa wetu kwa Mara nyingine Tena, kabla ya kufunga mwaka na kuingia mwaka Mwingine ni vema tupitie Hili jambo!!

    Apps Bora kwa Mwaka 2017 je nizipi hizo???
Hebu Tuzitame Ila kabla hatujazitazama hizo Apps Hebu tuangalie Vigezo na masharti kwanini ziitwe Apps Bora za mwaka!!

Google playstore Kila mwisho wa mwaka hutoa Matokeo au Takwimu Kuhusu Apps Na games zilizopendwa zaidi katika mwaka /zilizokuwa Bora zaidi.

Inasemekana Njia hii ya kutoa Apps Na games bora za mwaka hufanya Developers wengi wa Apps kuongeza Zaidi vitu vizuri katika Apps zao Ili kutengeneza Kilichobora na kuingia katika List ya Apps Bora za mwaka!!

 •Je unatizo lolote Au unahitaji msaada  Tafadhari Tuandike katika Email Yetu Bofya hapo Chini katika Hio picha!!
VIGEZO NA MASHARTI  KUITWA APPS BORA!

•Rating katika App husika lazima App hio iwe na Rating kuanzia 4.1 na kuendelea.

•Idadi ya Walio download App hio ndani ya mwaka huo
•App kufanyiwa Cheking ili kufix tatizo kwa Haraka
•Developer kutovunja sheria Ya masharti yake Na Google
•Jinsi ilivyo bora Pamoja na Mandhari.
•Wingi wa maoni ya watu wakisifia App  hio.
Zifuatazo ni Apps 6 Bora kwa mwaka 2017.
  1: ACTION direct-VIDEO EDITOR


Download ^^^
  Action Director -Ni moja kati ya App bora kabisa katika mwaka 2017 ,App hii inahusika na Masuala ya video edit  Ni nzuri pia ni rahisi kutumia na Inaeleweka Vizuri kabisa ,  Cha bora zaidi inapatikana Bure kabisa.

2:ADOBE PHOTOSHOP
Adobe Photoshop -Imechaguliwa Tena katika list ya App bora kwa Mwaka 2017 ikumbukwe hata mwaka 2016 App hii ilichaguliwa tena katika Orodha ya App Bora zaidi kwa mwaka huo., App hii inahusika na masuala ya Photo editor Ni bora kabisa pia Ni rahisi kuielewa!! Inapatikana Bure kabisa!!


3:OneTalk -TurboOneTalk Ni App bora kabisa katika List ya mwaka 2017 ,App hii inahusika na Masuala ya Message  Ipo kama Messenger Ni Nzuri inamuonekano murua pamoja na Yote hayo inapatikana Bure Kabisa!! 


4:PHOTO MATH                                                                                                  

 App hii inahusika na Masuala ya Hesabu ni Moja kati ya Apps Bora zaidi Katika soko. 
Matumizi ya App hii Inamsaidia mwana Hesabu kutoumiza kichwa pindi afanyapo Hesabu zake kwani App hii imerahisisha kila kitu. 

Jinsi ya kuitumia. 

1:Andika swali lako la Hesabu katika Karatasi ambalo limekushinda 
2:Chukua simu yako ya Smatphone  Na fungua App ya photo math
3:Baada ya kuifungua App hio Itafungua Camera Automatic Hivo utakacho takiwa kukifanya wewe Ni Kuweka camera vizuri huku ikilenga lile swali lako uliloandika katika karatasi yako. 
App hio itatoa Majibu ya swali lako papo hapo!!!. 

Uzuri wa App hii
1:Huihitaji kuwa na Data yaani unatumia Offline! 
2: Haihitaji Uwe na uelewa zaidi ndipo uitumie Kila kitu kipo Automatic!! 

Ijaribu leo Uone ilivo nzuri Na Nikweli lazima iwe katika list ya App  Bora kwa mwaka 2017.

5: SNAPCHART                                                                                                           
                                                                                                         

Ni App Moja nzuri kwa wale wapenzi wa kuchart na mitandao ya kijamii Snapchat nimoja ya mtandao ambao unakua kwa kasi siku hadi siku kutokana  na watumiaji kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana!!  Kiufupi kwa asiefahamu snapchart ni nini ni Social media kama ilivo Messenger au Facebook, instagram n.k ilasema Hii imekaa au inamuonekano wa kipekee!! 

6:GYROSCOPE                                                                                                     
Kwa Habari sahihi kuhusu hali ya hewa ya eneo lako tumia App ya Gyroscope ni App bora kabisa Katika mwaka 2017 
                           kwani inakupa taarifa sahihi Za Hali ya hewa ,taarifa ambazo hazina chenga wala longolongo nyingi.
 ijaribu leo ni moja katika APPS pendwa zaidi katika soko.
                       

Hizo ndizo App Bora kabisa kwa mwaka 2017 Ambazo google playstore Walizitambulisha katika list Zipo Apps bora nyingi ila hizo ndizo Zilizo Bora zaidi.