Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

5.11.17

Soma ujumbe huu Kabla ya kufungua Blog


Bara la Afrika linakuwa kwa kasi sana katika matumizi ya mitandao, mojawapo ya ukuwaji huo ni Tanzania pia,miaka ya hivi karibuni tumeona ongezeko kubwa la matumizi ya mitandao ya kijamii, inakadiriwa kuwa Watanzania milioni 8 watumia huduma za mtandao, kutokana na ukuaji huo pia vijana wengi wamejitahidi kufungua website na blog pia.
 Kitu cha kusikitisha ni kwamba ukuaji wa hizi blog ni wa kusua sua sana na mwishowe hufa.

             Kwanini zinakufa

Hizi blog zinakufa kwa sababu tu zimeanzishwa kwajili ya kupata pesa bila kuwekeza,yani mmiliki wa blog hazingatii ubora wa blog yake yupo tayari kupata matangazo ili aanze kupiga pesa,sasa asipopata basi anakata tamaaa na kuachana nayo.

           Wanakosea wapi?

Wengi wa wamiliki wa blog hizi wanakuwa na lengo moja tu kuingiza pesa kama mitandao mingine bila kuangalia kiwango cha machapisho yao,unakuta blog ina machapisho mengi lakini hayakidhi mahitaji ya msomaji,hii inapelekea kutoonekana hata kwenye ingini ya kutafuta ya Google.
       Kunakili bila kudadisi kwa undani

Hakuna kosa katika kunakili machapisho kutoka katika vyao vikubwa,shida inatokea blogger ananakili habari jinsi ilivyo na kuichapa hivyo hivyo bipa kupunguza chochote wala kuongeza kitu,yani kama mwandishi wa mwanzo kakosea nae ataweka kosa hivyo hivyo.
   
Kukosa AdSense ni Zimwi linalotafuna Blog nyingi

Kuna baadhi ya  wengine wameamua kuchapa habari kwa lugha ya kiingereza ili wapate kibali cha matangazo ya Google bila kuzingatia watembeleaji wanatoka wapi, mfano umetoa habari kutoka tovuti ya kingereza na ukaamua kuipost hivyo hivyo kwenye blog yako,ipi ya kwanza kuonekana kwenye search engine???....
Una blog ya kiteknolojia unatoa makala kwenye tovuti za kingereza na wewe unachapa hivyo hivyo kwa kingereza ilimradi tu upate AdSense ukishapata una watembeleaji 500 lakini miguso miwili (clicks) utatoka kweli??

         Ubinafsi kwa baadhi ya bloggers

Ubinafsi kivipi?unakuta mwandishi ni mmoja hawezi kumshirikisha kijana mwingine ili iwe na ufanisi zaidi,na mbaya zaidi inatokea pale anaposhirikishwa anaona kama dili nae anafungua ya kwake akijua ni rahisi tu,au pia pale wanapohitaji kushauriana wanakatishana tamaa.

  Ushauri wangu kwa mabloga wote Tanzania

Moja kati ya tovuti inayotembelewa kwa mara nyingi hapa Tanzania na nje ni ya millardayo.com huyu anaandika habari kwa kiswahili,kama kweli unataka kupiga pesa kwanini usichukue hizi habari kwa kiswahili na kuzichapa kwa kingereza? Je italipa au kupoteza muda bure.....
Unaweza kuongeza maoni yako kwenye comment chini pia

 Makala hii imeandaliwa na Smatskills kwa msaada wa teknokona