Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

10.11.17

NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD STATUS ZA WHATSAPP

Usisumbuke kuwaomba watu wako whatsapp ambao wameweka status wakutumie status zao pale unapopenda status fulani.

 njia rahisi ya kuzipata status moja kwa moja kwenye simu yako pasipo kutumiwa.


Toa shaka kama unatumia mods za WhatsApp au Unatumia WhatsApp messenger kwani njia hii itakusaidia wewe kuweza ku chukua status hizo bila kumuomba mhusika wala kigezo cha aina ya Version ya WhatsApp yako endapo tu umeipenda status hiyo.

Kama una WhatsApp messenger na unatamani sana kupata njia itakayo kuwezesha kukusaidia kuchukua status kwa watu wako bila kuomba wakutumie.

                         


PIA SOMA >>

MAREKEBISHO KWENYE GB WHATSAPP


Mahitaji: ES File Explorer

1. Tazama Status za rafiki zako
2. Kisha nenda kwenye file, manager kutumia ES File Explorer,
3. Nenda moja kwa moja kwenye Folder la Whatsapp,
4. Bofya mistari mitatu mifupi sana sehemu ya juu mkono wa kushoto
5. Kisha bofya "show hidden files" kuiweka on.
6. Kisha rudi kwenye folder la Whatsapp utaona kuna folder lingine limeongezeka, limefifia ukilinganisha na mengine limeandikwa *.status*
7. Lifungue na humo utakuta picha zote ulizotoka kuzitazama kwenye status Whatsapp,
8. Hapa sasa select picha unayohitaji kuihifadhi (save) kwenye simu yako na bofya vidoti vitatu juu upande wa kulia na chagua "share",
9. Itakuja orodha fulani hivi,
10. Katika orodha hiyo chagua "ES Save to.." kisha chagua mahali unapohitaji hiyo status na mpaka hapo utakuwa umenaliza.
  Angalia video hii ili kuelewa zaidi

▫️ Kwa Mod za Whatsapp:
 Mod nyingi za whatsap zinakuwa na njia moja tena Rahisi tu za kuchukua status fata hatua hizo

1. Fungua status unayohitaji kuipakua (kuidownload).
2. Kabla haijapotea bonyeza vidoti vitatu kwa juu mkono wa kulia.
3 Chagua "Download". Mpaka hapo umemaliza itapakuliwa na kuhifadhiwa kwenye simu yako.

▫️ Smatskills ©2017