Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

9.11.17

NINI MAANA YA DATA ROAMING? FAHAMU HAPAKatika hali ya kawaida tunakuwa tunamiliki smartphone lakini hatujui kazi ya baadhi ya kazi ya sehemu zilizopo kwenye simu zetu.Leo hii nitaongelea nini maana ya DATA ROAMING!!!
Kama inavyoonekana hapo kwenye picha 👆👆👆,sehemu hii hupatikana settings/mobile/mobile network 

Hivyo bhasi nini maana ya DATA ROAMING? 
Kwa lugha nyepesi na ya kueleweka unaweza sema data roaming ni kisaidizi cha network ya simu yako pale utakapofika sehemu ambayo kuna network ambayo haitambuliki na nchi yako, pia na mtoa huduma wako. 

MFANO.
Hapa nchini Kwetu tuna aina 3 za network bands
1. 2g (GSM)
2. 3g( CDMA)
3. 4g (LTE)

Na hizi hutegemea na sehemu ambayo wewe mtumiaji wa network au simu upo.  Sasa mfano ukaenda SOUTH AFRICA ukifika kule mfano simu yako inatumia TTCL ukifika kule hutoweza tumia TTCL yako kwasabbu ya network security

Hivo bhasi ili uweze tumia network service ya south Africa utawasha DATA ROAMING na kuendelea kutumia line yako...ila tu utakatwa makato kutokana na matumizi yako.

DATA ROAMING HAPA TANZANIA 
Katika hali ya kawaida data roaming hapa tanzania tunaweza sema haijakamata asilimia kubwa ya watu ambao wanatumia hii huduma. Lakini tumejaribu kufuatilia na kufanya uchunguzi kwa kutumia SONY EXPERIA Z1F tumegundua hii service inatumia frequency 900.  Hivo mtumiaji anayetumia huduma hii internet yake iko speed kuliko yule ambaye hatumiii. Kwasabbu data roaming kwa mujibu wa uchunguzi wetu ni COMBINED NETWORK ambayo mtumiaji hata akiwa kwenye network ya 2g speed yake itakuwa vilevile tofauti na yule ambaye hatumiii. Hivo bhac data roaming ni muhimu kwa upannde wa speed ya internet pamoja hapa kwetu hutotozwa gharama yoyote ila tu itafanyakaz huduma hii mahali ambapo ukiwa na network mbovu.

KWANINI?
Hii ni kwasababu ukiwa umewasha data roaming hapa tanzania unakuwa unaiforce simu iwe connected kwenye service hata kama network ipo 2g hivo speed ya network itakuwa palepale sasa hii tunaita advantage. Kwasababu mtumiaji ataweza tumia network hata kama eneo lililomzunguka lina 2g.

Swali.
NINI FAIDA NA HASARA ZA DATA ROAMING? 
A) faida
Data roaming inafaida hasa kwa pale ukiwa kwenye network mbovu yani (2g) wewe mtumiaji utaendelea kutumia simu yako kama kawaida na speed ile ile tofauti na mtumiaji wa kawaida.

. Pia huuumpa mtumiaji uhuru pale endapo akiwa kwenye aina ya network ambayo haitambuliki na mtoa huduma wake

B)HASARA
hasara kubwa ya data roaming ni kwamba makato yake yapo juu endapo ukienda nchi tofauti na nchi yako.

Pia huwezi share network yako.  Mfano ukiwa na data roaming mtu akitaka kuconnect wifi network yako, itafail kuconnect ila wewe unaweza kuconnect kwenye wifi yake

Kwa nchi kama Ethiopia ipo limited na ukitaka kutumia unlimited lazima utumie vpn kama express vpn,  cyberghost na n.k

Hivo bhac ndugu zangu na wapenz wa blog yetu nadhani kidogo umepata uelewa kuhusu data roaming. Ukiwa na swali tia comments zako pia unaweza tumia live chat yetu.

PIA USIKOSE SOMO LIJALO TUTAONGELEA DATA USAGE NINI KIFANYIKE UWEZE KUJIWEKEA MPKA WA MATUMIZI YA MB ZAKO.

@ahsante

Smatskills 2017