Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

26.11.17

Jinsi ya kuficha picha na video zako bila apps(hide)

    Katika ulimwengu wa simu janja kumekua na utandawazi sana,simu ina mambo mengi muhimu na mengine ya siri zaid.
   Ni kawaida unapompa mtu simu yako na sehemu ya kwanza kwenda inaweza kuwa kwenye matunzio yako(Gallery).

   Wengi wamehangaika kuwema app za kuficha (hide) baadhi ya video na picha zao lakini kikwazo kinakuja pale simu inapokua ina uwezo mdogo wa kuweka app za ziada.
   Leo SmatSkills tunawapa njia rahisi sana ya kuficha mambo yako bila ya mtu kuona wala hakuna haja ya kuweka pini.

SOMA PIA.    RUDISHA ACCOUNT YAKO YA FACEBOOK AMBAYO IME HAKIWA.

SOMA PIA.   JINSI YA KUFICHA DATA NA MAFAILI YAKO MTANDAONI [BACKUP]


Hatua ya kwanza nenda kwenye file manager unda folda maalumu kwa picha na video zako za siri, mfano (videozangu) baada ya kuunda kachague vitu unavyotaka kuficha huenda kutoka kwenye kamera au popote,ukishachagua hamishia kwenye folda videozangu, baada ya kumaliza kuhamisha,rename(lipe jina jipya) hilo folda yaani unapolipa jina andika hivi .videozangu
Mfano wa kuunda folda la kificho

 Piga Done hapo hautaona tena kwanzia kwenye file manager hadi kwenye matunzio (Gallery).
 
        UKITAKA KUZIONA JE?
ingia kwenye file manager bofya dot tatu upande wa kulia na utaona show hiden file(onyesha file zilizofichwa) hapo yatatokea mafaili yote yaliyofichwa katika muonekano huu.
File zilizofichwa zikiwa zimefifia kwa mbali

Unaweza kukagua kuangalia na hata kuongeza nyingine, baada ya hapo rudi kule juu Kafiche file zako na uendelee na mambo mengine.

Kama una swali karibu tukusaidie, usisahau kushare kwa ndugu na marafiki zako,kama una Telegram unaweza kujiunga nasi hapa SmatSkills
Usisahau kutufuatilia kwenye mitandao ya kijamii yote @smatskills