Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

27.10.17

Vigezo Muhimu Kabla hujanunua Simu

Kila kukicha simu janja[smartphone] zinauzika sana  zinatoka mpya  zinaboreshwa na zina maumbile ya kila aina,

   Je ni kitu gani muhimu cha kuangalia kabla ya kununua?

 hapa itategemea na mapenzi yako mwenyewe,kumbuka hakuna simu inayoweza kuja na kila sifa uitakayo.
Wanachofanya haya makampuni ya utengenezaji wa simu hawatakuwekea vigezo vyote lazma ukute kuna kasoro angalau hata moja,

  SIFA MUHIMU


 • Ujazo wa disk
 • Ram
kwanini ni muhimu,ni muhimu kwa sababu unaweza kununua simu kuubwa lakini ikawa haina uepesi wa kufanya kazi zako haraka,pia unaweza kununua simu kubwa na nzuri lakini ukaweka vitu vichache na kujaa, hapo umeona umuhimu wa hivyo vitu viwili juu hapo.

vionjo vinavyotofautisha simu

 • Diski uhifadhi
 • Ram
 • Kamera
 • Betri mAh[uwezo wa betri]
 • Toleo endeshi la kisasa[latest version]
 • Spidi ya mtandao[3G/4G]
 • Prosesa inayotumia
 • Pesa yako
 • Kampuni


  Mimi nataka kununua simu ni  simu gani itanifaa?

 • Hapa kama wewe ni muuza sura yani unapenda upigaji picha lazima uegemee kwenye KAMERA
 • kama unachezea sana simu [kucheza games,kuangalia movie na kuchat sana egemea kwenye BETRI
 • kama unapenda kwenda na wakati lazma uchague toleo la kisasa yaani LATEST VERSION
 • kama  unapenda kuweka vitu vingi utachagua DISKI UHIFADHI
 • kama unapenda kuperuzi haraka mtandaoni angalia  SPIDI YA MTANDAO
      MAJUTO

usipoangalia vigezo hivyo unaweza kununua simu na baada ya muda ukaichoka kwa sababu haina kigezo fulani,huenda ulipendea Kamera kumbe haikai na chaji,au ulipendea ukaaji wake na chaji lakini kumbe haina 3G.

Baada ya kuangalia vigezo vyote hivyo sasa utageukia mfuko wako na  unaweza kuchagua kampuni unayotaka,kama kuna kilichosahaulika unaweza kutuachia kwenye maoni chini hapo.
 usosahau kushiriki na nduguzo ili nao waweze kufaidi uchambuzi kama huu