Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

25.10.17

Umeroot simu yako???lazima uwe na hizi Apps

Kama unataka  uhuru mwingi kwenye simu yako basi lazima uroot simu.kwanini ni muhimu???
SOMA HAPA👉 Faida ya kuroot simu
sasa ukiwa umefanya hivyo nimekuandalia programu tumizi bora sana kwa ajili ya simu yako

      1.Lucky Patcher:- hii ina umaarufu sana japo si kwa watu wote, umaarufu wake umeongezeka baada yavwatu kuitumia kuhack (kudukua)games mbalimbali na kupata coin za bure,ambapo bila hivyo itakulazimu ununue kwa pesa,lakini ukiwa na Luckypatcher umemaliza,kazi zingine ni

 • Kusanidua(Uninstall) apps
 • Kublock ads
 • Kubackup apps n.k


    2.Titanium Backup:- 

hii ni zaidi ya msaada,kwani usipokuwa na hii pale unapotaka kubadili rom yako au unapotaka kurest simu yako utakosa kila kitu,ukiwa na Titanium backup itakusaidia kuokoa mpaka data za ndani ya app,yan kama WhatsApp unaweza kubackup hadi mazungumzo.

     3.Quick Boot 

hii inarahisisha kuboot simu yako haraka tofauti na kushikilia vitufe kama cha kuwasha na cha kuongeza sauti,ukiwa na quick boot huna haja ya kushikilia batan.

    4.Flashify :- huenda wengi wasiifaham kutokana na utumizi wake,hii ina kazi kazaa kama
 • Kuflash roms
 • Kuweka recovery za CWM
 • Kubackup system nzima ya simu yako n.k 


    5.AdBlock Plus:- jina lenyewe linajitambilulisha,kuna kero sana kwenye matangazo hasa yake yanayofunika kioo kizima cha simu,sasa ukiwa umeroot simu yako huu mzigo unakufaa sana.

    6.Boot Animations:- hii ni maakumu kwa wale wnapenda mambo mengi kwenye simu zao,boot animation ni ile logo inayoonekana simu unapowaka,yani kama ni Tecno, Huawei, Samsung n.k kaz ya hii app ni kubadili na kuweka zingine uzitakazo.

    7.ES File Explorer:- huyu ndio baba wa file manager,hakuna kitu isichoweza kufanya hii app moja wapo ya kazi zake ni kama

 • Kubackup
 • Kufuta app yeyote mahali popote
 • Kuinstall app kwenye system
 • Kubadili font
 • Kushare file baina ya kifaa na kifaa
 • Kuficha file/apps n.k sifa ni nyingi sana 


    8.Link2SD

hii ni kwa zile apps korofi zisizo taka kwenda kwenye SD card sa hapa lazma zikubali tu, hakikisha umeroot simu yako na ipe simu yako nafasi kwa kuhamisha viti kwenye memry card.

    9.Xposed Framework

hii haifanyi kazi yenyewe kuna plug in yake inaitwa Gravity Box ,ndani ya box hili kuna makorokoro mengi sana ambayo ukiyatumia vizuri utajiona kama unatumia toleo la kisasa la Android kumbe ni la zamani, mfano kama unatumia Android 5.lollipop ukatafuta Gravity Box ya android 6 marshmallow unaweza kutumia module za Android 6 kwenye 5 yako na muonekano ukawa kama 6.

   10.iFont:- hii ndio maarufu kuliko zote,kwanza ndio app inayoshawishi Vijana wengi kuroot simu zao ili tu waweze kubadili font mbalimbali kama za Samsung,hii inajieleza yenyewe kwaio haina maneno mengi.

Kama a kuna swali niandikie kwenye uwanja wa Comment chini hapo na nitajibu haraka iwezekanvyo, kama umependa makala hii fanya kushiriki na ndugu na marafiki zako kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii