Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

21.10.17

JINSI YA KUTAFUTA SIMU ILIYOIBIWA

Inasikitisha na kuhuzunika pale utakapo ibiwa simu yako au kupoteza,kwanza kabisa unajiuliza nianzie wapi niweze kuipata,uchungu huongezeka zaidi pale utakapopiga na simu kuita. unaweza kufikiria mengi simu hiyo Hadi kwa waganga watakuja kwenye mawazo.
Sasa leo hakuna haja ya kuwaza sana,ntakupa njia japo si tegemeo sana lakini unaweza kuokoa simu yako hata baadhi ya vitu muhimu kama imei namba na hata ukafuta data zako, ukipata imei unaweza kupeleka TCRA wakaifunga pia lakini njia ingine hii....

               Mobile Tracker Free

Hii app haipo kwenye soko la Android (playstore) hii app ina mambo mengi sana hizi ni baadhi ya sifa zake muhimu

  • Kusoma msg kwenye simu yako
  • Kufuatia mawasiliano (kupiga/kupigiwa)
  • Inakagua picha
  • Inakagua mitandao ya kijamii
  • Unarecod sauti, video
  • Live viewing
Sifa ni nyingi sana.
  Watu wasio kuwa waaminifu wamekuwa wakitumia isivyo(kudukua wenzao)
Umuhimu mwingine wa kutumia app hii,unaweza kuwa una kijana wako ambaye ana simu janja lakini hutaki aitumie vibaya,kwa kumwekea app hii unaweza kujua kila kitu kijana wako anatumia kwenye simu yake,na unaweza kufunga (block)baadhi ya app ambazo unaona sio nzuri kwake.
   Unaweza kuipakuwa hapa 👉MTF
Baada ya kupakiwa unajiandikisha ili kuwa na akaunti kwenye mtandao wao baada ya kujiandikisha na kufanya mipangilio yote app itakuwa haionekani (hiden) kwenye mtiririko wa app zako,nini cha kufanya utapiga *1234* hapo itafunguka.
Ukimaliza kila kitu unaweza kuingia kwenye dashboard yako na kukagua shughuli zote kwenye simu uliyoweka
Fuatana nami katika video hii ili kuelewa zaidi kwanzia mwanzo hadi mwisho.Kumbuka unaweza kuingia sehemu yeyote kwenye kifaa chochote.
Una swali niandikie kwenye comment chini hapo au pia unaweza kujiunga na kundi letu la Telegram SmatSkills kwa maswali zaidi na maujanja mengine.