Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

16.10.17

Blackberry waachia simu mpya [Blackberry Motion]

Hii ni full touch (mguso kote) tofauti na mwanzo walikuwa wakitoa simu ambazo ni mguso na kicharazio(keyboard) naona wamebadilisha upepo baada ya kuona kicharazio hakina nafasi tena

 Hizi ni baadhi ya sifa za Blackberry Motion.


BlackBerry Motion inakuwa pia moja ya simu zenye betri la ujazo mkubwa, betri lake ni la mAh 4,000. Simu hii pia inakuwa simu ya kwanza kubeba jina la BlackBerry yenye uwezo wa kuhimili muda mrefu ndani ya maji bila madhara yeyote.
      Sifa nyingine.     • Kioo/display ya ukubwa wa inchi 5.5 (Resolution 1080 x 1920 – FHD)
  • Pia Display yake ina ubora wa juu dhidi ya ukwanguaji (Premium anti-scratch), hivyo unaweza weka simu pamoja na funguo bila shida.
  • Prosesa ya Snapdragon 625 SoC pamoja na GB 4 ya RAM
  • Teknolojia ya Quick Charge 3.0, hii ikimaanisha inaweza chaji hadi kufikia asilimia 50% ndani ya dakika 40
  • Jumba la simu ni la aluminiamu na hivyo usihofu kuhusu kudumu kwa simu
  • Inakuja na toleo la Android 7.1 Nougat ila kufikia 2018 itapata toleo la Android 8.0 Oreo.
  • Kamera ya Megapixel 8 kwa selfi na kamera ya megapixel 12 kwa nyuma. 

                                     Chanzo ni Teknokona