Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

18.10.17

APPS KUMI MUHIMU KWENYE SIMU YAKO

Soko la simu janja limekuwa kubwa sana hasa hapa Tanzania na Afrika pia,kila mtu ananunua hizi simu kwa lengo lake binafsi,huenda ukanunua kwa sababu za kibiashara, matumizi tu ya kawaida.
  Je ni apps gani muhimu ambazo hutakiwi kuzikosa kwenye simu janja yako??? Kama unasoma uchambuzi huu kwa makini kuna kitu utafaidi sana.


  1.     True Caller:-hii ni app itakayokusaidia kujua majini ya nambari mpya zisizo na majina,kwa nini ni muhimu? inakera sana pale mtu anapokupigia simu na kumuuliza nani mwenzangu??wakati namba ulikuwa nayo huenda imefutika ulipobadili simu. Ukiwa na true caller huwez kumuuliza mtu unaitwa nani. True Caller                                                                                                
  2.    WiFi Map:- hii inafanya kazi kubwa sana na ni muhimu sana,ukiwa na hii itakusaidia kujua ni wapi kulipo na wifi public na kukuonyesha namba zake za siri(passiward). Kwaio unaweza kuwa na simu janja lakini huna salio la MB.ondoa shaka ukiwa na WiFi Map                                      
  3.    Photos:- hii inakuja na karibu simu zote za android isipokuwa zile za (Chinese Version) huenda hujawahi tumia au hujui kazi yake, ukiwa na photos ondoa shaka kuhusu kupoteza picha zako, ukinunua simu yako cha kufanya ingiza akaunti ya ya barua pepe na nenda kaset (auto backup) kwanzia hapo piga picha uza simu hata kama umeibiwa simu bado picha zako      utazikuta katika simu utakayonunua kama simu yako haina unaweza kuipakua Photos                      
  4.    Keep:- hii ni huduma nyingine kutoka Google,kama unavyojua Google hawajawahi kukosea,ukiwa na keep itakupa faida ya kuhifadhi taarifa zako muhimu kama ujumbe mfupi, historia na hata kuandaa baadhi ya historia au dokumenti mbalimbali,nimekuwekea video hapa jinsi unavyoweza kuandaa.Keep                                                                                                                   
  5.  WPS Office:-hii inakuja na simu nyingi sana saivi lakini wengi hawajui matumizi yake,basi hii ni muhimu sana kwani ukiwa na hii utaweza kusoma aina zote za mafaili mbali mbali kama doc,pdf,text n.k na sio kusoma tu bali utaweza pia kuunda zako kwa kutumia hii app WPS  Office.[unaweza pia kuangalia video juu ili kujua zaidi namna ya kuitumia]              
  6.   Shazam:-hapa nimegusa upande wa burudani, huenda ukasimbuka sana kujua au kuufahamu nyimbo uliyosikia inapiga sehemu,unataka kujua jina la msanii jina la nyimbo na hata video yake,ukiwa na shazam husumbuki kumuuliza mtu (nyimbo hii inaitwaje) itakua ni aibu sasa        Shazam
  7.     ES file explorer:- japo simu zote zina file manager lakini kuna faida kutumia ES,ina kazi nyingi sana nitakupa chache tu-kuficha app na picha,kuokoa app(kubackup),kusaidia OTG kebo kuonekana kwa simu ambazo hazina uwezo huo,tena ukiwa umeroot ndio faida lukuki.     ES file
  8.    Screen Record:-hapa sitakupa app moja,zipo nyingi kati ya hizo kuna Du Recorder,mobizen n.k,kwanini ni muhimu kuwa na hizi app?? utaweza kurekodi kioo cha simu yako na kutuma video hiyo kwa rafiki au ndugu yako anaetaka labda umwelekeze kitu fulani kwenye simu,ili kuepuka kuonea sana utarekodi kioo chako na kumtumia kama video.DU Recoder                        
  9.  VPN:-hizi zipo nyingi sana,kuna za kulipia na zingine za bure,kazi yake ni nini? hizi zina kazi ya kudanganya sever unayotumia na kukuunganisha na ingine,yani kuna baadhi ya vitu fulani mtandaoni havipatikani katika nchi fulani lakini kwa kutumia VPN utaweza kupakua au kuangalia[mfano China facebook,google na baadhi ya apps zimefungiwa]sasa ukiwa kule ukitumia VPN unatumia tu.Master VPN
  10.   Translate:-huu ni mzigo mwingine kutoka Google,hii ni muhimu sana kwa kila mtu,kwanini?ukiwa na hii itakusaidia kutafriri lugha zote na sio kwa maandishi tu hata kwa picha,mfano umeona tangazo sehemu lakini umeshindwa kulielewa kutokana na lugha hata heruf zake,ukiwa na Translate utaweza kupiga picha na kusoma kwa lugha utakayo.Translate