Pata ujuzi, uchambuzi, habari za kiteknolojia na apps za kijanja ukiwa na smatskills, kuwa karibu ili ujifaidi mwenyewe

Breaking

29.9.17

JINSI YA KUTENGENEZA ANDROID APPS BILA KUTUMIA LUGHA YA COMPYUTA (CODES) 2017


Ulimwengu kwa sasa umekua sana kiasi kwamba karibia huduma zote unazipata kupitia simu yako ya mkononi, hii imesababisha watoa huduma wote ambao hutoa huduma mtandaoni kulazimika kutengeneza programu (App) kwaajili ya huduma zao, lakini katika kufanya hivyo bado unakutana na changamoto kwani ni lazima kuajiri watu kwaajili ya kufanya hivyo ndio mana leo nmekuletea njia hii ya kutengeneza app za android bila kuwa na ujuzi wowote maalum.

Kumbuka hauitaji ujuzi mkubwa kufanya hivi bali unaitajika kuwa na kompyuta yenye uwezo wa kuunganisha internet pamoja na logo na picha mbalimbali za kuweka kwenye programu yako. Ni vyema kuangalia kwanza matumizi kisha ndipo ujue jinsi ya kutengeneza picha na logo za kuweka kwenye App au programu yako, pia ni vizuri kuwa na simu ya android kwaajili ya kutest programu yako kabla ujaamua kuipost kwenye masoko ya Android kama Play Store au Amazoni Store.


Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa ili kutengeneza programu hii ni vyema ukajua unataka kutengeneza programu ya aina gani zifuatazo ni tovuti 10 zitakazo kuwezesha kutengeneza programu mbalimbali kutokana na maitaji yako, lakini sisi tutatumia tovuti ya Adromo kama mfano wetu wa leo.

Mobile Roadie
TheAppBuilder
Appy Pie
AppMachine
BiznessApps
BuzzTouch
Good Barber
Kinetise
Andromo
Como DIY
Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya Andromo kisha tengeneza akaunti kwenye tovuti hiyo, hakikisha unatumia email au barua pepe ambayo utaweza kuingia kwa muda wowote hii ni muhimu sana kwani programu yako itatumwa kwenye barua pepe hiyo baada ya kumaliza kutengeneza programu hiyo, hivyo hakikisha unatumia email sahihi.

Baada ya kujisajili na kuhakiki akaunti yako ingia kwenye akaunti yako kisha utaona mahali palipo andikwa Create New App bofya hapo kisha utaletewa sehemu ya kujaza jina la project hapo hakikisha una andika jina la programu yako kisha bofya Create, baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ulio andikwa Your App Activities hapo utatakiwa kuweka aina ya vitu ambavyo unataka programu yako ifanye, vitu vyote vinapatikana kwa kubofya sehemu iliyoandikwa Add an Activities ifuatayo ni list ya vitu ambayo utatumia na kazi zake.

About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
Audio Player – Hapa utaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
Contact – Hapa utaweza kuweka anwani yako
Custom Page – Hapa utaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
Email – Hapa utaweza kuweka barua pepe
Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
HTML Archive – Hapa utaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
Map – Hapa utaweza kuweka ramani
PDF – Hapa utaweza kuweka file la PDF
Phone – Hapa utaweza kuweka namba ya simu
Photo Gallery – Hapa utaweza kuweka picha mbalimbali
Podcast – Hapa utaweza kuweka mfumo wa Podcast
RSS Feed – Hapa utaweza kuweka RSS fee ya blog yako
SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
Twitter – Hapa utaweka ukurasa wao wa Twitter
Website – Hapa utaweka tovuti yako
YouTube – Hapa utaweka ukurasa wako wa Youtube

Chagua aina ya kitu ambacho unataka programu yako ifanye kisha jaza vitu utakavyo ulizwa kisha endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya Style hapo utaweza kuchagua rangi pamoja na aina ya style ambayo unataka programu yako iwe, baada ya hapo endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya dashboard hapo utaweza kuchagua aina ya dashbord unayotaka kutumia kwenye app yako kisha save alafu endelea mbele kwa kuchagua Service tumeruka Monetize kwa sababu kwa hii ni app ya bure hivyo hutoweza kuweka matangazao mpaka hapo utakapo lipia kwenye tovuti hiyo kwa maelezo zaidi bofya hapa.

Tukirudi kwenye sehemu ya Service weka namba yako ya Google Analytics ili kujua watu wangapi wanaangalia vitu kwenye programu yako, kisha nenda hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza app yako, sehemu hii inapatikana kwenye Build chagua sehemu hiyo kisha chagua sehemu


Baaada ya kusoma hio ndio check video hiii hapa


 BAADA YA HAPO FUATANA NAMI KWENYE SEHEMU YA KWANZA HII HAPA CHINI


BAADA ya kumaliza sehemu ya kwanza katika somo letu ENDELEA NA SEHEMU YA PILI HII HAPA CHINI
SEHEMU YA  TATU   HII HAPA CHINI


malizia na SEHEMU YA NNE NA UANZE leo kutumia application yako bila shida yoyote SEHEMU YA NNE HII HAPA CHINI


AHSANTENI SANA , kama ukikutana na shida yoyote usisite kutujuza kupitia comments hapo chini .
@SMARTSKILLS
@2017